Latest in Tech

Hospitali ya Kenya kuwatibu wagonjwa wa Uganda

Mashine ya kutibu ugonjwa wa saratani ilioharibika
Hospitali moja nchini Kenya imeahidi kuwalipia matibabu wagonjwa wa saratani kutoka nchini Uganda kufuatia kuharibika kwa mashine inayotibu ugonjwa huo nchini Uganda.

Hospitali ya chuo kikuu Aga Khan imesema katika taarifa kwamba inaweza kutibu idadi ndogo ya wale wanaohitaji uuguzi.

Serikali ya Uganda tayari ilikuwa imetangaza kuwa itawasafirisha wagonjwa hao kupata matibabu nchini Kenya.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes