kuu wa jeshi linalomuunga mkono
kiongozi wa waasi Riek Machar, bwana Simon Gatwech Dual amewasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba.
Kuwasili kwake kunaibua
matumaini ya kufufuka kwa harakati za kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba
wa amani uliotiwa sahihi yapata miezi 8 iliyopita.
Kamanda huyo Gatwech Dual aliwasili kutoka Ethiopia akiandamana na kikosi cha wanajeshi 100.
Hiki
kilionekana kuwa ni kikwazo kikubwa kwa kiongozi wa waasi kuweza
kurejea Juba ambapo alisisitiza kuwa lazima kwanza awasili Gatwech,
wanajeshi pamoja na silaha.
Msemaji wa waasi alisema Machar sasa atarejea Juba kesho
Machar,
ambaye aliondoka juba wakati vita vya wenywe ka wenyewe vilipoanza
Desemba mwaka wa 2013, anatarajiwa kuunda serikali ya umoja na mpinzani
wake mkuu Rais Salva Kiir.
Machar anatarajiwa kurejea na kukabidhiwa wadhfa wa
makamu wa rais baada ya kufutwa na rais Kiir miezi michache kabla ya
machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kutibuka.
Kwa sasa, Machar yuko katika kambi ya waasi karibu na mpaka wa Ethiopia.
Itambidi
avuke hadi Ethiopia, kwa uwanja wa ndege ambao uko karibu, katika
maeneo ya Gambela, ili aweze kupanda ndege ya kuelekea Juba
Msemaji
wa waasi William Ezekiel amenukuliwa akisema kwamba wapiganaji wa
Machar wapatao 195 pamoja na mkuu wa majeshi Simon Gatwech Dual amabao
wamewekwa chini ya vikwazo na Marekani na Umoja wa Mataifa, pia walikuwa
wanatarajiwa kurejea Juba hii leo.
Ezekiel amelaumu kuchelewa
kurejea kwa Machar mjini Juba kutokana na wahisani ambao walikuwa
wanafadhili msafara wake kujiondoa.
Maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya milioni mbili kutoroka makwao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Vita hivyo vimeibua uhasama mkubwa wa kikabila na ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Marekani,
Uingereza na Norway ziliungana kupitia mchakato maarufu kama Troika, na
wamekuwa wakitoa misaada kwa ajili ya amani nchini Sudan Kusini,
zikisema kwamba pande zote mbili lazima zionyeshe nia ya dhati ya kuleta
amani.
Ubalozi wa Uingereza unasisitiza kwamba kurejea kwa Machar ni muhimu sana katika mchakakato wa kuunda serikali ya Umoja
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment