Maafisa wa kijeshi wa Korea kusini wanasema
Korea kaskazini imefyatua kombora hilo kutoka Wonsan, eneo lililo kambi
ya jeshi mashariki mwa pwani ya Korea Kaskazini.
Inaamika
kuwa jaribio hilo lilikuwa la pili la makombora ya Korea kaskazini la
masafa ya wastani inayojulikana kama Musudan, ambayo yana uwezo wa
kufika katika vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika kisiwa cha
Guam katika bahari ya Pasifiki.
Lakini utawala wa Pyongyang hauna nguvu kwa sasa ya kutumia makombora hayo.
Jaribio jingine la makombora hayo mwezi uliopita, halikufanikiwa baada ya kombora hilo kulipuka muda mfupi baada ya kurushwa.
Kumekuwa
na wasi wasi kuwa utawala wa Pyongyang umekuwa ukiimarisha uundaji wa
zana zake za nyuklia, kabla ya kufanyika kwa kongamano kuu la chama
tawala mwezi ujao.
Mkutano huo unadhamiria kuonyesha mamlaka ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye, ameonya kuwa korea Kaskazini itawekwa vikwazo zaidi ikiwa itaendeleza majaribio hayo.
'Ikiwa
korea kaskazini itaendelea na majaribio zaidi ya nuklia, itakuwa
inafanya uchochezi na kukiuka sheria za kimataifa kama ilivyoidhinishwa
na azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa tangu ilipofanya
jaribio lake la nne. Tutakumbwa na hali tofauti sana kuliko ilivyo sasa,
kwa sababu korea kaskazini imekuwa ikifanya majaribio hayo kwa muda wa
miaka mitatu'.
Vikwazo zaidi vya kimataifa viliwekea kora
kaskazini baada ya majaribio hayo ya makombora ya masafara marefu ya
nuklia mwaka uliopita.
Home » SAYANSI NA TEKNOLOJIA » Korea kaskazini yafyatua kombora la pili
Korea kaskazini yafyatua kombora la pili
By Unknown • 09:36:00 • SAYANSI NA TEKNOLOJIA • Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment