![]() |
| assad |
Takriban watu 65 wamefariki katika
milipuko ya mabomu kadhaa katika maeneo muhimu ya pwani yanayodhibitiwa
na serikali ya Syria ,ripoti zinasema.
Milipuko ilikumba miji ya Tartus na Jableh.Milipuko kadhaa ilisababishwa na walipuaji wa kujitolea muhanga,kundi moja la uchunguzi limesema.
Vyombo vya habari vya Syria vinasema kuwa vituo vya mabasi ni miongoni mwa maeneo yaliolengwa .
![]() |
| Ngome za Assad zalipuliwa |
Mashambulio kama hayo si kawaida katika eneo hilo.Hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza milipuko hiyo.



Post a Comment