Watu wanafaa kutumia dawa aina ya
aspirin mara tu baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi ili kuzuiya
athari zaidi zinazosababishwa na ugonjwa huo,watafiti wamesema.
Wanasayansi
kutoka chuo cha Oxford wanasema kuwa ijapokuwa madaktari wameagizwa
kutoa dawa hiyo kwa wagonjwa,umuhimu wa kuitumia mapema umepuuzwa na
matibabu hucheleweshwa.
Wakiandika katika jarida la la afya la Lancet ,wametaka maelezo yalio sahihi kuhusu utumizi wa dawa hiyo. Ugonjwa wa kiharusi hutokea wakati kuna muingilio wa
damu inayoelekea katika ubongo ,na husababisha mikono na miguu
kudhoofika mbali na kutatiza mtu anapozungumza huku ishara zake
zikipotea katika kipindi cha siku chache.
Lakini uwezekano wa ugonjwa huo kukukabili na nguvu huwa juu siku chache baada ya kumkabili mwathiriwa.
Post a Comment