Sherehe ya kila mwaka ya kula mbwa imeanza kusini mwa taifa la China licha ya pingamizi kutoka katika taifa hilo na ugenini
Takriban mbwa 10,000 na paka wanatarajiwa kuuawa na kuliwa wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi inayofanyika Yulin.
Wanaharakati
wanasema kuwa hafla hiyo ina ukatili huku wale wanaotaka sherehe hiyo
kupigwa marufuku wakiandikisha saini milioni 11. Mamlaka ya eneo hilo inasema kuwa sherehe hiyo
haiungwi mkono moja kwa moja na serikali lakini hufanywa na
wafanyibiashara wa kibinafsi.
Je,sherehe hiyo inahusu nini?
Sherehe
hiyo ya mlo wa nyama ya mbwa huwaleta pamoja watu wengi katika eneo la
Yulin ili kujichagulia nyama ya mbwa, matunda na vinywaji. Utamaduni wa kula nyama ya mbwa ulianza miaka 500
iliopita nchini China,Korea Kusini pamoja na mataifa mengine ambapo
wengi wanaamini mlo huo huondoa joto mwilini wakati wa majira ya
kiangazi.
Post a Comment