Latest in Tech

MICHEZO

SIASA

VIDEOS

Latest Updates

Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

MAMBO 10 MUHIMU YA KUZINGATIA UKIWA NA MTOTO CHINI YA MIAKA MITANO

00:37:00
                                                           
                                                                                           
wanaawake wengi wakishajifungua hupenda kuishi kwa mazoea au uzoefu hasa kwa kufuata bibi na mama wanasema nini kuhusu afya ya mtoto, sio vibaya lakini ni vizuri uwe makini sana kwani maisha yamebadilika sana na kuna mambo mengi yamepitwa na wakati na mengine ni hatari kiafya hivyo usikubali kila unachoambiwa na watu bila kukichuja.
kuna mambo kadhaa ya msingi sana ambayo usipokua makini nayo utampoteza mtoto kama ifuatavyo.
hakikisha anapata chanjo zote; ukiona unaambiwa mtoto anatakiwa achomwe chanjo fulani maana yake ugonjwa unaozuiliwa na chanjo hiyo umeshaua watoto wengi sana hivyo ukileta uzembe tu mtoto wako anaweza kua mmoja wa watakao uwawa na ugonjwa huo.
mpeleke hospitali akiugua; mara nyingi akina mama hunza kutibu wenyewe na wakiona mtoto amezidiwa kabisa ndio wanakimbia hospitali, mara nyingi watoto hawa wanapona kwa bahati tu lakini wengi hufariki..mtoto sio kama mtu mzima akiugua kidogo tu anafariki hivyo usilete uzembe katika hili.
tumia neti ya mbu; kama wewe neti huiwezi basi nunua kitanda maalumu cha mtoto usiku akilala alale na net, malaria inaongoza kwa kuua watu hapa afrika na watoto wakiuawa zaidi kuliko hata watu wazima.
kula vizuri mlo kamili; ili upate maziwa ya kutosha yenye virutubisho vyote hakikisha unakula vizuri kwa kufuata mlo kamili yaani mchanganyiko wa vyakula vyote, kipindi mtoto ananyonya achana na mawazo ya kupungua uzito, subiri afikishe miaka miwili ya kunyonya ndio uanze kupungua lakini pia mifupa, nyama na kila kitu cha mtoto kinatokana na wewe hivyo kula vizuri kurudishia madini yaliyopotea wakati wa ujauzito...usipozingatia hili utakutana na upungufu wa madini siku za usoni
osha matiti yako kila ukitaka kunyonyesha; akina mama wengi wana shughuli nyingi hatukatai lakini tabia ya kunyonyesha bila kuosha matiti wakati wa shughuli hizo ndio chanzo cha mtoto kuharisha mara kwa mara. ukitoka kwenye shughuli zako oga au osha matiti afu ndio umpe mtoto anyonye.
fuata ushauri wa daktari; usipende kutoa dawa hovyo bila kupata ushauri wa daktari au muhudumu wa afya, dawa hizo hutolewa kwa uzito na mara nyingi uzito wa mtoto huongezeka kila mara hivyo dozi aliyopewa miezi mitatu iliyopita huenda mwezi huu haimtoshi tena.
achana na maziwa mbadala; kama hauna jinsi labda wewe ni muathirika wa ukimwi na umekatazwa kunyonyesha au hauna maziwa ya kutosha basi unaweza kumpa mtoto maziwa ya ngombe au maziwa ya dukani lakini nikuthibitishie kwamba maziwa ya mama hayana mbadala wa 100%, yale ya mama ni bora zaidi kwa afya ya mwili na akili za darasani hapo baadae.
weka hatari zote mbali na mtoto; mtoto asipelekwe jikoni kwenye moto, usiweke dawa zozote mahali pa wazi yaani dawa za panya, dawa za binadamu na kadhalika, nyumba yako hakikisha haina shimo hata moja na hakikisha mtoto hachezi barabarani yaani hatari zote weka mbali.
simamia maendeleo ya mtoto; baadhi ya wanawake wako bize sana na maisha baada ya kujifungua hivyo kazi ya kulea huwaachia wafanyakazi wa ndani, ni hatari sana kukabidhi maisha ya mtoto wako kwa mfanyakazi..jitahidi uende clinic hata mara moja moja ujue maendeleo yakoje, jifunze jinsi ya kusoma kadi ya clinic kujua kama uzito unapanda au unashuka, rudi nyumbani ghafla ukague kama mtoto anapewa chakula kama unavyotaka.
kua makini usibebe mimba mpya kabla huyo mdogo hajakua; kunyonyesha tu kunaweza kuzuia mimba lakini kama mama ananyoshesha zaidi ya mara kumi kwa siku ndani ya miezi sita ya kwanza kama huwezi kutumia kalenda au damu hazijaanza kutoka basi chagua njia ya uzazi wa mpango ambayo ni salama kwa mtoto.

NJIA 10 ZA KUJITIBU UCHOVU WA POMBE {HANGOVER}

23:49:00

hangover ni nini?
hii ni hali ya kujisikia vibaya inayowapata watu watu ambao wanakua wamekunywa pombe nyingi jana yake, dalili zake ni kuuma kichwa sana, kutapika, kuishiwa nguvu, kujisikia uvivu sana na kushindwa kufanya kazi.
hali hii huvumilika mara nyingi lakini wakati mwingine hali hua mbaya kiasi kwamba mtu huweza kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi.
sasa wewe kama mywaji wa pombe ni vizuri ukazifahamu njia ambazo unaweza kuzitumia kutibu hangover kabla au baada kunywa pombe kama ifuatavyo.
kunywa maji mengi;maji ni matibabu makuu ya hangover kabla na baada ya kunywa pombe, kawaida pombe humfanya mtu akojoe sana na kupoteza maji mengi mwilini na hii ndio moja ya sababu kuu ya kupata hangover sasa kitaalamu ili kuzuia hangover unatakiwa unywe chupa moja ya pombe na glass moja ya maji kila wakati na ikitokea hukufanya hivo na umeamka asubuhi una hangover basi jitahidi unywa hata lita tatu mpaka nne siku hiyo.[angalizo;usinywe maji yote kwa pamoja, weka kwenye chupa unywe taratibu]

kula chakula chenye mafuta mengi kabla ya pombe; chakula kama nyama, samaki, kuku, sambusa na vingine hua na mafuta mengi...pombe ikikuta mafuta tumboni inapata tabu kufanya kazi haraka kuliko ikikuta tumbo halina kitu, hii huzuia hangover za kesho yake lakini ukishakunywa haikusaidii tena.
kunywa kahawa; kawaha kitaalamu inaitwa stimulant, hii ni nzuri kwako ambaye umeamka na hangover lakini una kazi za kufanya siku hiyo zinazohitaji umakini mkubwa hivyo kahawa itakuondolea uchovu na kukufanya uwe makini lakini kunywa na maji pia kwani kahawa hufanya mtu akojoe sana kama pombe.
meza dawa za maumivu; maumivu ya kichwa yakiwa makali kuna dawa unaruhusiwa kumeza kupunguza maumivu hayo mfano diclofenac, aspirin, ibuprofen...usinywe paracetamol au dawa yeyote yenye mchanganyiko wa paracetamol kwani ikiungana na pombe inaharibu maini
                                                             
fanya mazoezi; kama kichwa hakiumi sana fanya mazoezi yeyote kwani hii itakusaidia kupunguza pombe mwilini, na kukuletea mood ya kufanya vitu kwani ubongo hutengeneza homoni ya furaha yaani endorphine wakati wa mazoezi.
epuka kuzimua na pombe; huu msemo hutumika na walevi kwamba anaamka na pombe ili kuondoa pombe, hapana hii haifai kabisa kwani inaweza kukuletea ganzi mwilini na kukufanya uwe mtegemezi wa pombe kwenye maisha yako yaani bila kunywa pombe huwezi kufanya chochote.
                                                 
ongeza sukari mwilini;pombe hupunguza sana sukari mwilini na hii ni kwasababu maini
yanashindwa kutengeneza sukari ya ziada na kua bize kuondoa pombe mwilini hivyo unaweza kunywa juisi, soda au kula chakula. juice ni nzuri zaidi kwani hurudisha na madini yaliyopotea mwilini.
kunywa tangawizi na maji ya moto; chukua tangawizi isage kisha ichemshe na maji ya moto, hii itakuondolea kichechefu na kukuletea hamu ya kula.
rudi kulala; mara nyingi pombe huharibu mfumo wa usingizi hivyo mtu anaweza asipate usingizi wa kutosha kwa kushtuka ovyo usingizini, lala mpaka utakapoona usingizi umeisha ndio uanze shughuli zingine.
jiuepushe na mwanga mkali na sauti kubwa za kelele; mtu akiwa katika hali hii hawezi kuvumilia mwanga mkali na sauti kubwa hivyo kaa mbali navyo kupata nafuu.
                                                       

Utafiti: Uchu wa ngono Sweden washuka

05:53:00
Taifa la Sweden linazindua utafiti wa miaka mitatu kuhusu maisha ya ngono ya raia wake.
Habari zimechapishwa katika jarida moja zikisema kuwa raia wa taifa hilo wanashiriki ngono kwa kiasi kidogo.
Waziri wa Afya Gabriel Wilkstrom amesema kuwa iwapo msongo wa mawazo ama maswala mengine ndio tatizo la watu kushiriki ngono kwa kiasi kidogo basi hilo pia ni swala la kisiasa.
Amesema kuwa huku jamii ikihusishwa na ngono katika kila kitu kuanzia matangazo,mitandao ya kijamii na katika maisha ya kila siku,swala hilo linakabiliwa na aibu na kutokuwepo katika mjadala wa kisiasa .

Je Kuna Madhara Msichana Akifanya Mapenzi Wakati Akiwa Katika Hedhi (Siku zake)?

07:18:00
Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala mwanamke kama kati yao hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa.

Ila kama mmoja wapo ana ugonjwa wa zinaa, huo ni wakati wa hatari sana kwa maambukizi, kwa sababu utando ndani ya mfuko wa uzazi unabomoka na mlango wa mfuko wa uzazi unakuwa wazi. Hivyo ni rahisi sana vijidudu vya magonjwa mbalimbali kuingia mwilini mwa msichana. Vilevile kama msichana tayari ameambukizwa na magonjwa ya zinaa, katika damu yake viko vijidudu vingi vinavyoweza kumwambukiza mvulana.

Kwa sababu mara nyingi ni vigumu kufahamu kama kati ya wapenzi hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa, haishauriwi kujamii ana wakati wa hedhi na kama ndivyo basi kondomu itumike.

Katika jamii nyingi kujamii ana wakati mwanamke yuko wenye hedhi haikubaliki kwa sababu ya mila au dini.

Utafiti: Harufu ya kuku inazuia Malaria

06:44:00
Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria ?
Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha,, Fuga kuku !
Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.
Watafiti nchini Ethiopia na Sweden wamegundua kuwa mbu wanaobeba virusi visababishavyo ugonjwa wa Malaria huwa wanafanya kila wawezalo kukaa mbali na ndege huyo anayefugwa majumbani.
Moja kati ya majaribio katika utafiti huo ilijumuisha kumweka kuku aliyehai karibu na mtu aliyelala chini ya chandarua kinachozuia kuumwa na mbu.
Image copyrightJAMES GATHANY CDC
Image captionHarufu ya kuku inazuia Malaria
Mwaka uliopita watu laki nne 400,000 walikufa kutokana na ugonjwa wa malaria barani Afrika, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Japo idadi na visa vya maambukizi ya Malaria vinaendelea kushuka, wataalamu wanaendelea kutafuta mbinu bora zaidi ya kuangamiza kabisa ugonjwa huo.
Vimelea vya malaria hujificha ndani ya maini kabla ya kuambukizwa kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi mwengine kupitia kwa mbu wa kike anayefyonza damu.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Malaria umebaini kuwa mbu hunusa harfu ya mnyama kabla ya kumuuma.
Image captionUtafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.
Hata hivyo hawajui nini katika harufu ya kuku inawapa kinyaa mbu .
Katika hatua ya pili ya utafiti huo sasa, watafiti hao wanalenga viungo vya harufu ya kuku ilikuunda kinga dhabiti dhidi ya mbu hao wanaoambukiza malaria.
Habtie Tekie kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa Ethiopia anasema kuwa mipango inaendelea na huenda majaribio yakatekelezwa karibuni.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sweden walihusika katika utafiti huu.
Iligundulika kuwa idadi ya mbu ilipungua kwa asilimia kubwa sana mahala popote ambapo viungo vya kuku vilitumika ima ni manyoya ama sehemu zingine za kuku.
Wanasayansi wanasema kuwa kuna haja ya kuendelea kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na mbu kwani hata sasa mbu wanaonesha dalili ya kuwa sugu dhidi ya madawa yaliyoko sasa.

Rihanna afuta ziara akihofia virusi vya Zika

03:48:00
Mwanamuziki wa kizazi kipya Rihanna amekataa kutumbuiza mashabiki wake nchini Colombia kwa kuhofia kuambukizwa virusi vya Zika.
Waandalizi wa tamasha la Lollapalooza Colombia wamejipata taabani baada ya kipusa huyo kukataa katakata kuhudhuria tamasha hilo licha ya kuwa maelfu ya mashabiki walikuwa tayari wamekwisha nunua tiketi zao.
Wanamuziki wengine waliopaswa kutumbuiza katika tamasha hilo Lana Del Rey, Disclosure, The Chainsmokers na Wiz Khalifa.
''Baada ya kujiondoa kwa nyota wa muziki wa Pop Rihanna, hatuna budi kufutilia mbali tamasha zima, hata hivyo tunawaomba radhi mashabiki wetu kwa tukio hilo na tungependa kuwahakikishia nyote kuwa gharama ya tiketi zote zilizokuwa zimenunuliwa zitalipwa.''

Image copyrightREUTERS
Image captionRihanna alikuwa ametarajiwa kufungua makala ya kwanza ya tamasha la Lollapalooza Colombia

Msemaji wa Lollapalooza Colombia aliwaambia wahandishi wa habari za burudani.
Japo Rihanna hakuwa ametajwa rasmi kuwa mwanamuziki huyo aliyelazimisha tamasha hilo kufutiliwa mbali Waandalizi wa tamasha hilo wamewataka wafadhili wao wawawie radhi kwa sababu ambazo hazingeepukika.
Aidha tamasha hilo la Lollapalooza Colombia lilikuwa limeratibiwa kufanyika katika mji mkuu wa Bogota, Colombia.
Shirika la Afya duniani WHO lilitangaza ugonjwa wa Zika kuwa janga la umma mnamo mwezi februari mwaka huu baada ya mlipuko wa maradhi hayo nchini Brazil na haswa eneo zima la kusini mwa Marekani.

Image copyrightEPA
Image captionVirusi vya Zika havimdhuru mtu wala kumsababishia maradhi lakini virusi hivyo vimeonesha madhara makubwa kwa wanawake wajawazito

Tahadhari hiyo ya shirika la afya duniani liliibua hofu miongoni mwa wanariadha wanaopaswa kushiriki katika michezo ya Olimipiki mjini Rio De Janeiro kuanza mwezi ujao nchini Brazil. kitovu cha maambukizi hayo.
Virusi vya Zika havimdhuru mtu wala kumsababishia maradhi lakini virusi hivyo vimeonesha madhara makubwa kwa wanawake wajawazito ambao wengi wamejifungua watoto wenye vichwa vidogo kuliko inavyopaswa.
Aidha virusi hivyo vimebainika kusalia katika manii ya wanaume kwa muda mrefu.

Mtoto apandikizwa pua mpya India

03:45:00
Madaktari nchini India wamepandikiza pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la uso.
Pua ya Arun Patel iliharibika alipougua ugonjwa wa homa ya kichomi
Maambukizi hayo yaliharibu pua yake akiwa mtoto mdogo.
Upandikizaji kama huo ulifanywa nchini China mwaka 2013 ambapo mtu mmoja ambaye aliharibu pua yake katika ajali alipewa pua mpya.
Wazazi wa Arun walimchukua na kumpeleka katika daktari mwengine katika kijiji cha jimbo la kati la Madhya Pradesh ambapo aliugua kichomi mda mfupi baada ya kuzaliwa.
Image captionUpandikizaji
Lakini matibabu aliyopewa yaliongeza hali yake na hivyobasi kupoteza pua yake.
Miaka kadhaa baadaye,kundi moja la madaktari katika mji wa Indore liliamua kufanya upasuaji usiokuwa wa kawaida ambapo Arun alipata pua mpya.

Magonjwa ya akili yakithiri Sudan Kusini

03:43:00
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema maelfu ya raia wa Sudan Kusini wanasumbuliwa na kiwewe baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, na walio wengi hawana matarajio ya kupata tiba.Shirika hilo limesema watu walilazimishwa kula nyama ya binaadamu wenzao na wengine walilazimishwa kuipasua miili ya binaadamu wenzao wakati huo wa kivita, vilivyoanza mwishoni mwa mwaka 2013.
Amnesty inasema kwamba katika hali ya kusikitisha Sudan Kusini ina hali mbaya ya ukosefu wa huduma za afya ya akili, ikiwa na madaktari wawili tu magonjwa ya akili wakihudumia idadi ya watu zaidi ya milioni kumi.
Wagonjwa wa magonjwa ya akili mara nyingi wamekuwa wakizuia magerezani.
 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes