Latest in Tech

MICHEZO

SIASA

VIDEOS

Latest Updates

Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

Huu ndo ujio mzito na mpya wa Ray C kimuziki

08:03:00





Kutoka Kushoto: Anna Peter wa East Africa Radio, Ray C na Mamy Baby wa Clouds FM

Miaka minne iliyopita, kwa hali aliyokuwa nayo, kila mtu alimkatia tamaa kuwa ndio basi tena ameshatumbukia kwenye shimo waliloshindwa kutoka vijana wengi. Matumizi ya madawa ya kulevya yalimuongezea jina la uteja lililolifunika jina lake la utani ‘kiuno bila mfupa.’ Rehema, msichana mrembo aliyekuwa ndoto ya wanaume wengi, akapoteza thamani yake.
Jina lake likapotea kwenye ramani ya muziki na akawa mtu wa kuonewa huruma. Na kwa jinsi madawa ya kulevya yalivyo, humnyong’onyeza mtumiaji, humpunguzia utimamu wake kiakili, humpa utegemezi unaotesa yasipotumiwa na ikawa wakati mwingi Rehema akawa wa kukutwa amezima! Maskini wa Mungu Ray C akaingia kwenye dimbwi la maji ya moto ya uteja, nani wa kumuokoa?
Kwa alama aliyoiweka kwenye muziki wa Tanzania kwa nyimbo kibao zilizofanya vizuri, Ray C akapata msaada kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa zaidi nchini, Rais Jakaya Kikwete. Alijitolea kumpeleka rehab, kumsadia kwa hali na mali hadi hali yake ikarudi kwenye mstari – walau kwa muda huo. Aliingia kwenye mpango wa kutumia methadone aliodumu nao kwa takriban miaka mitatu.
Katika kipindi hicho, Ray C akageuka kuwa kinara wa vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya. Alianzisha pia taasisi yake, The Ray C Foundation kwaajili ya kampeni za kukemea ubwiaji unga. Katika kipindi hicho, Rehema, alijaribu tena kurejea kwenye muziki kwa kuachia wimbo mmoja ‘Mshum Mshum’, ambao hata hivyo haukufanikiwa kumrudisha pale alipokuwa ameishia.
Haikuwa rahisi kuishinda vita hiyo na mwaka huu alionekana kuweka silaha chini kwa kudaiwa kurejea tena kwenye matumizi ya madawa hayo. Video iliyosambaa mtandaoni akionekana akiwa kwenye mvurugano wa akili, akilia na kutaka kujichoma kisu, ilirejesha tena hofu kwa wapenzi wa muziki kuwa amerudi kwenye jela ya uteja.
RAY C ANARUDI
Peleka mbele hadi wiki moja iliyopita, Ray C anaonekana kupata chaji ya muziki inayompeleka hadi kwenye studio za kisasa za Wanene Entertainment. Kwanza nimefurahi kuona amebadilika mno kutoka yule msichana aliyenenepa hadi kuupoteza utambulisho wake. Amerudisha umbo lake la zamani linalompa matumaini ya kulikomboa jina la jukwaani – kiuno bila mfupa.

Uhakika nimeupata kwenye video alizoziweka Instagram zikimuonesha akiwa kwenye mazoezi makali ya kucheza huku kiuno chake kikifuata vyema maagizo kinayopewa. Huu unaweza kuwa urejeo wenye nguvu zaidi wa muimbaji huyu na namuomba Mungu amsaidie kukaa tena kwenye nafasi yake.
Muziki wa Tanzania unamhitaji Ray C hasa kwakuwa kuna upungufu wa wasanii wakubwa wa kike. Inanipa moyo kuona mahaba yake ya muziki yamerudi kwa kasi ya ajabu. Napata amani nikimuona anavyofurahia mchakato wa kutengeneza nyimbo mpya. Nafarijika kuona kuwa amezungukwa na watu wanaotaka arudi kwenye chati.
Atakachohitaji baada ya hapo ni kuungwa mkono na vituo vyote vya redio nchini na pia mashabiki wakitimiza wajibu wao. Yapaswa kukumbuka kuwa muziki pekee ndio unaweza kuwa mkombozi kwake na unaoweza kumpa nafasi ya pili – nafasi ya kung’ara tena.
Naamini anarekodi nyimbo nyingi na katika hizo lazima kutakuwa na nyimbo kubwa. Pamoja na matatizo yote aliyoyapita, sijawahi kuwa na shaka na kipaji chake. Nasubiri kwa hamu kusikia kile alichotuandalia.

VIDEO: TAZAMA UWEZO WA RAPA HUYU WA KIKE MWENYE UMRI WA MIAKA 13 ALIYESAINI SONY MUSIC

11:27:00
Lebo kubwa ya muziki Epic/Sony records wamefanya usajili mkubwa wiki hii baada ya kupata saini ya rapa Luis Rivera Jr Aka Lil Poopy mwenye miaka 13.

Lil Poopy alikuwa msanii wa French Montana kwenye kundi lake la Coke Boys na kutoa mixtape iliyopewa jina “Coke Aint A Bad Word“.
Album hii ilileta matatizo kwenye familia ya Lil Poopy na baba yake mzazi kuchunguzwa na polisi baada ya mtoto wake mwenye miaka 13 kuimba kuhusu Wanawake, dawa za kulevya ,ngono na magari ya thamani.

Msanii huyu anafananishwa na wasanii kama Bow wow,Lil Romeo na Taylor Swift walioanza muziki wakiwa wadogo.

Hii ndo list ya wasanii wanaotajwa kuwania tuzo za BET Hip-Hop 2016

06:04:00
Tuzo za hiphop za BET ziko njiani na tayari wametangaza wasanii wanaowania tuzo hizi kwenye vipengele tofauti, Kwa miaka mitatu mfululizo Drake ametajwa kuongoza kwenye vipengele vingi zaidi anavyowania msanii yoyote, Drake anawania tuzo kwenye vipengele 14 ambavyo ni kama Album of the Year, Track of the Year,na MVP of the Year.
Msanii Future anawania vipengele 10 ambavyo ni kama Album of the Year, Best Mixtape, na Made-You-Look Award kwa Best Hip-Hop Style.
DJ Khaled anawania vipengele 9 na Kanye West 8.
BET Hip-Hop Awards zinafanyika jumamosi ya  Sept. 17 kwenye ukumbi wa Cobb Energy Performing Arts Centre mjini Atlanta,na kuonekana kwenye tv Oct. 4
Orodha kamili ndio hii ya tuzo za BET Hip-Hop 2016.
Best Hip-Hop Video
2 Chainz – “Watch Out”
Desiigner – “Panda”
DJ Khaled feat. Jay Z & Future – “I Got the Keys”
Drake – “Hotline Bling”
Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared – “All the Way Up”
Kanye West feat. Rihanna – “Famous”
Best Collabo, Duo or Group
DJ Khaled feat. Drake – “For Free”
DJ Khaled feat. Jay Z & Future – “I Got the Keys”
Drake & Future – “Jumpman”
Drake feat. Wizkid & Kyla – “One Dance”
Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared – “All the Way Up”
Best Live Performer
Drake
Future
J. Cole
Kanye West
Kendrick Lamar
Lyricist of the Year
Chance the Rapper
Drake
J. Cole
Kanye West
Kendrick Lamar
Video Director of the Year
Benny Boom
Colin Tilley
Director X
Hype Williams
Kanye West
DJ of the Year
DJ Drama
DJ Envy
DJ Esco
DJ Khaled
DJ Mustard
Producer of the Year
DJ Mustard
Dr. Dre
Metro Boomin
Mike WiLL Made-It
Pharrell Williams
MVP of the Year
DJ Khaled
Drake
Future
Kanye West
Kendrick Lamar
Track of the Year
“All the Way Up” – Produced by Cool & Dre and Edsclusive (Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared)
“Controlla” – Produced by Boi-1da (Drake)
“Hotline Bling” – Produced by Nineteen85 (Drake)
“I Got the Keys” – Produced by Southside (DJ Khaled feat. Jay Z & Future)
“Panda” – Produced by Menace (Desiigner)
Album of the Year
DJ Khaled – I Changed A Lot
Dr. Dre – Compton
Drake – Views
Fetty Wap – Fetty Wap
Future –DS2
Kanye West – The Life of Pablo
Best New Hip-Hop Artist
Anderson .Paak
Bryson Tiller
Chance the Rapper
Desiigner
Tory Lanez
Hustler of the Year
DJ Khaled
Drake
Future
Jay Z
Kanye West
Made-You-Look Award (Best Hip-Hop Style)
A$AP Rocky
Drake
Future
Kanye West
Nicki Minaj
Best Mixtape
Chance the Rapper – Coloring Book
French Montana – Wave Gods (Hosted By Max B)
Future – Purple Reign
Lil Uzi Vert – Lil Uzi Vert Vs. The World
Young Thug – Slime Season 3
Sweet 16: Best Featured Verse
2 Chainz – “No Problem” (Chance the Rapper feat. Lil Wayne & 2 Chainz)
Drake – “Work” (Rihanna feat. Drake)
Kendrick Lamar – “Freedom” (Beyoncé feat. Kendrick Lamar)
Kodak Black – “Lockjaw” (French Montana feat. Kodak Black)
Nicki Minaj – “Down in the DM” – Remix (Yo Gotti feat. Nicki Minaj)
Impact Track
J. Cole – “Love Yourz”
Jay Z – “Spiritual”
Jidenna – “Long Live the Chief”
Raury feat. Key – “Trap Tears”
Sir The Baptist feat. ChuchPeople – “Raise Hell”
People’s Champ Award
Desiigner – “Panda”
DJ Khaled feat. Drake – “For Free”
Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared – “All the Way Up”
O.T. Genasis feat. Young Dolph – “Cut It”
Travis Scott – “Antidote”
Young Thug – “Best Friend”

Picha: alikiba kuachia video kali mpya akiwa na warembo hawa wakali

10:12:00
Alikiba yuko mbioni kuachia silaha yake mpya. Staa huyo wa ‘Aje’ ameonjesha kidogo kile kitakachoonekana kwenye video ya ngoma yake mpya, na mashallah itakuwa na warembo haswaaa.Staa huyo ameshare picha akiwa mbele ya jumba la kifahari na warembo wanane jijini Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa huko mwezi uliopita.
Pia ameshare video akiwa na video queen aitwaye, Michaela Roy.

Fiesta Mwanza kumdondosha Wizkid

07:25:00

Clouds FM wamethibitisha kumdondosha hitmaker huyo wa ‘Shabba’ Jumamosi, August 20.


“Kituuuuuuu #DealDone kwa mara ya kwanza ndani ya Mwanza #StarBoY wako @wizkidayo utatapata kumshuhudia LIVE juu ya jukwaa la #Fiesta2016 #Imooooo,” wameandika Clouds.
Hii itakuwa mara ya pili muimbaji huyo anakuja Tanzania. Mwezi October mwaka jana alitumbuiza kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Hiki ndicho kiasi cha Pesa alichokuwa akilipwa Hanscana na Wanene Entertainment.

06:57:00
Kama ulikuwa una shauku ya kujua kiasi cha pesa ambacho muongozaji wa video nchini Hanscana alikuwa analipwa na studio za Wanene,uongozi wa studio hizo wametaja kiasi walichokuwa wakimlipa director Hanscana.
Akiongea kwenye kipindi cha funiko base,Gentriez ambaye ni mmoja watu wa ndani wa kampuni hiyo amesema Hascana alikuwa analipwa sjilingi milioni mbili kila mwezi na studio hizo na pia video zote alizokuwa akizifanya pesa zilikuwa zinaingia kwa Hanscana.
Wanene tulikuwa tunamlipa mshahara hata kabla kampuni haijafunguliwa tulikuwa tunamlipa na video alizokuwa akifanya pesa yote ilikuwa inaingia mfuko kwa Hascana kwa hiyo wanene walikuwa wamewekeza kwake lakini baada ya kufungua kampuni ilibidi kwenye kila kazi lazima kuwe na percent ya kampuni..tulikuwa tunamlipa milioni mbili kwa mwezi” alifunguka Gentriez

Rapa Young Thug abadilisha jina lake la kimuziki

06:52:00
Rapa mwenye mikogo tofauti kwenye muziki ,tabia na mavazi yake Young Thug amesema anampango wa kubadilisha jina lake na kujiita  ‘No, My Name Is Jeffery
Young Thug anategemewa kutangaza jina hili jipya muda wowote sasa kwa mujibu wa mmiliki wa lebo ya 300 ‘Lyor Cohen‘.
Jeffery imetajwa kuwa album mpya ya Young Thug yenye mastaa kama Elton John, Birdman, Swizz Beatz, na Floyd Mayweather.
Jeffery Lamar Williams ndio jina halisi la Young Thug na leo August 16 amefikisha miaka 25.

The Game ajitamba kuwa amelala na dada wote watatu wa Kim Kardashian.

06:46:00
Rapa The Game amejitamba kuwa amelala na dada watatu wa Kim Kardashian ila mpaka sasa hajawataja kwa majina. Kupitia wimbo wake mpya wa “Sauce,” The Game anasema amelala na Kardashians watatu .
Kwenye mtari huu The Game anasema “I used to f*** bhes that Usher Raymond passed off / Then I fed three Kardashians – hold that thought.
Kwenye wimbo huu “Sauce” into iliyotumika ni ya Dj Khaled na mwisho wa wimbo anasema “I got 99 problems, but the sauce ain’t one.” Game yupo studio akifanya album yake ya 1992,

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes