Afisa wa kijeshi wa cheo cha juu
nchini Korea Kaskazini, ambaye alikuwa akisimamia masuala ya ujasusi
ameihama nchi hiyo na kuelekea Korea Kusini.
Shirika la habari la Yonhap nchini Korea Kusini, lilinukuu taarifa zilizosema kuwa kanali huyo alitajwa kuwa shujaa na wale walioihama Korea Kaskazini.
Zaidi ya watu 28,000 wameihama Korea Kaskazini tangu kumalizika kwa vita vya Korea, lakini kuhama kwa maafisa wa vyeo vya juu si jambo la kawaida,.
Wiki iliyopita raia 13 wa Korea Kaskazini waliokuwa wakifanya kazi kwenye mikahawa nchini humo, walihama kwenda Korea Kusini kwa pamoja.
Shirika la Yonhap linasema kuwa wanasiasa kadha wa vyeo vya juu wamehama kwenda Korea Kusini siku za hivi majuzi wakati wakifanya kazi nchi za ng'ambo.



Post a Comment