Vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini
vimekamilisha shughuli ya kurejea mji mkuu wa Juba, kama sehemu ya
mpango wa amani uliotiwa sahihi kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe
vilivyodumu kwa muda wa miaka miwili unusu.
Wanatarajiwa kumhakikishia usalama kiongozi wa waasi Riek Machar, ambaye aliteuliwa kuwa makamu wa rais kwenye serikali ya mpito na ambaye anatarajiwa kuwasili Juba mwezi Ujao.
Mapigano yamewalazimu zaidi ya watu milioni 2.2 kukimbia makwao, katika taifa hiyo janga zaidi duniani tangu mwaka 2103.
Post a Comment