Aliyekuwa kasisi wa Italia ambaye
alizuiliwa mateka nchini Ufilipino kwa miezi sita, ameondoka hospitalini
baada ya kuachiliwa huru.
Msemaji wa jeshi nchini humo amesema haijulikana ikiwa wanamgambo hao walilipwa kikombozi ili kumuachilia huru.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa kundi hilo lililipwa zaidi ya dola laki sita .
Kundi la Abu Sayyaf limefahamika kwa vitendo vyake vya kuwateka nyara raia wa kigeni na kuitisha kiasi kikubwa cha pesa ili kuwaachilia huru.
Post a Comment