ESPERANCE KUTUA LEO KWA NDEGE YA KUKODI TAYARI KUIVAA AZAM FC
Kikosi
cha Esperance de Tunis ya Tunisia inatarajia kuwasili nchini leo Ijumaa
kwa ndege binafsi ya kukodi kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Azam FC
huku ikificha idadi ya watu katika msafara wao.
Azam
inatarajia kuvaana na Esperance katika mchezo wa Kombe la Shirikisho
Afrika, mechi ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, keshokutwa
Jumapili.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saadi Kawemba, amesema wapinzani wao hao watatua leo usiku na kufikia katika Hoteli ya Bahari Beach.
“Hawajatutaarifu
watakuja na kikosi cha watu wangapi kwa kuwa watajihudumia wenyewe,”
alisema Kawemba ambaye wiki iliyopita alisema kuwa Esperance wakifika
wao Azam watawahudumia kila kitu kwa kuwa wamekubaliana makubaliano
maalum ili nao wakienda Tunisia wawahudumie pia.


Post a Comment