Bondia Conor McGregor ameibuka mshindi dhidi ya Nate Diaz kwenye pambano la UFC 202 lililofanyika wikiendi hii.
Ushindi huo ni kisasi cha McGregor dhidi ya Diaz aliyemshinda kwenye pambano lao lililopita.
Mahasimu hao walikumbatiana baada ya pambano kuisha na kushuhudia Diaz akienda chini mara tatu.
Diaz alionekana kuumizwa zaidi kwenye pambano hilo huku uso wake ukijaa damu. Diaz ametaka pambano la tatu.
Tazama picha zaidi:
Mchezaji na kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger, ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani, ikiwa ni majuma kadhaa baada ya timu hiyo kushindwa kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa sehemu ya mafanikio yaliyopatikana wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, ambapo Ujerumani walitwaa ubingwa wa fainali hizo katika ardhi ya Brazil kwa kuifunga bao moja timu ya taifa ya Argentina.
Schweinsteiger, ametangaza kustaafu soka la kimataifa huku akiacha kumbu kumbu ya kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani katika michezo 120 sambamba na kufunga mabao 24.
“Katika michezo 120 niliyocheza nikiwa na timu yangu ya taifa, sina budi kujivunia kwa mafanikio niliyoyapata na ninaamini kipindi hiki ni sahihi kwangu kutangaza kuachana na timu hiyo, ili kupisha wachezaji wengine,”Imeeleza taarifa ya Schweinsteiger.
Juventus wamemnunua mshambuliaji wa Agentina Gonzalo Higuain kutoka Timu ya Napoli kwa pauni milioni 75.5
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Juventus kukubali kutoa kitita hicho kinachokaribia Euro milioni 90 ambazo watazilipa kwa awamu.
Malipo hayo ya Mzaliwa wa Ufaransa Higuain aliyeanzia uchezaji wake wa kulipwa katika timu ya River Plate ya Argentina yanachukua nafasi ya tatu kwa ukubwa baada ya yale yaliyolipwa na Real Madrid walipomnunua Cristiano Ronaldo kwa Pauni milioni 80 na Gareth Bale kwa Pauni milioni 85.
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ambaye hivi sasa yupo likizo baada ya michuano ya Euro 2016, July 24 2016 alioneka akiwa Las Vegas, Marekani kwenye show ya Jennifer Lopez.
Ronaldo ambaye wiki kadhaa alikuwa katika fukwe za Ibiza, Hispania na familia yake akiwa katika boti ya kifahari, July 24 ameonekana akiwa na rafiki yake waki furahia katika show ya J.Lo kwa sasa Ronaldo bado anauguza jeraha lake la goti.
Video Ronaldo akiwa katika show ya J.Lo huko Las Vegas, Marekani
Meneja mpya wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola, amesema hatakuwa na tatizo lolote kumsalamia kwa mkono meneja wa Man U Jose Mourinho, wakat wa mechi kati ya vilabu hivyo mjini Beijing.
Mechi hiyo itakuwa ya pili kati yao tangu wote waache kufunza vilabu vya Barcelona na Real Madrid mwaka 2012. Wote wamekana tofauti zoa na Guardiola anasme kuwa atamsalamia kwa mkono kama njia ya urafiki.
Wakati Mourinho naye aliulizwa kuhusu suala hilo, pia alisema kuwa atamsalamia Guardiola kwa mkono.
“Nilifanya kazi naye kwa miaka mitatu huko Barcelona, Tumesimamia tofauti, uhusiano kati yetu ni wa kawaida, alisema Mourinho.
Beki wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal, Man City na Liverpool Kolo Toure, mwenye umri wa miaka 35, ametangazwa kusajiliwa na klabu ya Celtic ya Scotland kwa mkataba wa mwaka mmoja, hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa Kolo Toure kufundishwa tena na kocha Brendan Rodgers ambaye amewahi kumfundisha katika kikosi cha Liverpool.
Polisi nchini Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.
Video kuhusiana na tukio hilo, inamuonyesha mtu huyo akipigwa mieleka na walinda usalama, baada ya kuingia katika msafara wa watu na kuelekea moja kwa moja hadi kwa mtu aliyekuwa na mwenge huyo akiwa na nia ya kumpokonya.
Mtu huyu alinaswa na kuchukuliwa, huku mbio za mamani za mwenge huo zikiendelea muda mfupi baadaye.
Mwenge huo unatazamiwa kufika mjini Rio de Janeiro tarehe 4 mwezi ujao, kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano ya Olimpiki.
Polisi nchini Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.
Video kuhusiana na tukio hilo, inamuonyesha mtu huyo akipigwa mieleka na walinda usalama, baada ya kuingia katika msafara wa watu na kuelekea moja kwa moja hadi kwa mtu aliyekuwa na mwenge huyo akiwa na nia ya kumpokonya.
Mtu huyu alinaswa na kuchukuliwa, huku mbio za mamani za mwenge huo zikiendelea muda mfupi baadaye.
Mwenge huo unatazamiwa kufika mjini Rio de Janeiro tarehe 4 mwezi ujao, kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano ya Olimpiki.
Kocha mpya wa Man United Jose Mourinho ametaja orodha ya wachezaji wake watatu wa muda wote.
Mourinho amewataja Messi, Pele na Diego Maradona kama ndio wachezaji bora wa muda wote huku akiacha kumtaja Cristiano Ronaldo ambaye alitegemewa kuwepo kwenye orodha hio kutokana na uwezo wake toka amepata umaarufu chini ya klabu ya Man Utd.
Ronaldo amewahi kufundishwa soka na Mourinho kwa misimu mitatu katika klabu ya Real Madrid, mwaka 2012 alifanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or akiwa chini ya Mourinho,
Kocha wa Liver pool Jurgen Klopp amemsajili beki mpya kuja Liverpool kwa ada ya pound milioni £5. Beki huyu ni Ragnar Klavan na anatokea klabu ya Augsburg.
Ragnar Klavan ametia wini kwenye mkataba wa miaka mitatu na ataziba nafasi ya Martin Skrtel aliyehamia Fenerbahce na Kolo Toure.
Jurgen Klopp anamfahamu vizuri Klavan sababu mchezaji huyu amecheza kwenye ligi ya Ujerumani ya Bundesliga kwa miaka minne.
Ikiwa Manchester United wanaelekea kukamilisha usajili wa Paul Pogba kutoka klabu ya Juventus kwa ada pound milioni £100 ikiwa ndio rekodi mpya ya uhamisho kama itakamilika.
Man Untd walianza na ofa ya pound milioni £86 ila hata wakilipa hio badu malipo mengine na kodi itazidi ada waliyopokea klabu ya Tottenham ambayo ilikuwa pound milioni £85m wakati wa usajili wa Gareth Bale kwenda Real Madrid mwaka 2013.
Neymar hajajumuishwa orodha ya wachezaji kumi watakaoshindania tuzo
Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limetangaza orodha ya wachezaji kumi watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora Ulaya wa msimu wa 2015/16.
Orodha hiyo hata hivyo imewaacha nje wachezaji nyota wakiwemo Neymar kutoka Brazil.
Aidha, hakuna mchezaji yeyote anayechezea soka yake Uingereza. Jamie Vardy na Riyad Mahrez wanaochezea mabingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) Leicester City walikaribia sana kuwa kwenye orodha hiyo.
Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10 yametangazwa huku Cristiano Ronaldo akipewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo itakayotolewa Agosti 25 mwaka huu.
Majina hayo 10 yametangazwa baada ya kufanyika mchujo wa majina ya wachezaji 37 ambao walikuwa wamependekezwa awali na kupigiwa kura, ambapo UEFA imetaja majina ya wachezaji 10 waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ikiwa majina 27 ya wachezaji yaliingia katika kinyanga’nyiro hicho.
Image copyrightAFP
Majina ya wachezaji hao kumi ni Gareth Bale – Real Madrid, Gian-luigi Buffon -Juventus , Antoine Griezmann - Atletico Madrid, Toni Kroos - Real Madrid , Lionel Messi -Barcelona, Thomas Müller -Bayern Munich, Manuel Neuer - Bayern Munich , Laveran Ferreira Pepe - Real Madrid, Cristiano Ronaldo -Real Madrid, Luis Suarez –Barcelona.
Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Zlatan Ibrahimivic amemjibu nyota wa zamani wa soka, Eric Cantona kutokana na kauli yake ya siku chache zilizopita iliyodai kuwa mchezaji huyo hawezi kuwa mfalme ndani ya timu hiyo labda achague kuwa mtoto wa mfalme.
“Just one last thing, there can only be one King in Manchester. You can be the Prince if you want to. And the No 7 is yours if you are interested. That is my welcome gift to you… The King is gone! Long live the Prince!,” ulikuwa ni ujumbe alioutoa Cantona siku chache zilizopita.
Baada ya kauli hiyo, Ibrahimovic ameliambia gazeti la Aftonbladet, “I admire Cantona and I heard what he said.”
“But I won’t be King of Manchester. I will be God of Manchester,” ameongeza.
Wachezaji hao wote wawili wanajulikana kuwa na sifa ya utukutu huku Cantona aliondoka United akiwa hana maelewano mazuri na aliyekuwa kocha wake Ferguson na Ibrahimovic naye aliwahi kukwaruzana na Pep Guadiola wakati wapo Barcelona lakini pia aliwahi kufungiwa kwa kosa la kumpiga muamuzi.
Mwana soka anayetajwa kuwa mchezaji bora duniani Lionel Messi naye pia ameenda kupumzika kwenye visiwa vya Ibiza baada ya michuano ya Euro 2016 akiwa na familia yake,