Latest in Tech

KANYE WEST NA JAY Z WAFUNGULIWA MASHTAKA

kanye west na jay z
Baada ya mafanikio makubwa ya Kanye West kupitia album yake mpya ya The Life of Pablo iliyosikilizwa kwenye Mtandao wa TIDAL tu na kushika namba moja kwenye chati Billboard 200, shabiki amejitokeza na kusema amedanganywa kuhusu upatikanaji wa album hii.

Shabiki Justin Baker-Rhett amefungua kesi ya madai dhidi ya Kanye West, Jay Z’s S. Carter Enterprises na TIDAL  akidai TLOP ilitangazwa kupatikana kwenye mtandao wa TIDAL lakini baada ya yeye kulipa  apesa na kujiunga kwenye mtandao hio,album hii imewekwa kwenye mitandao mingine.

Kabla ya kutoka kwa album yake  Kanye alitangaza kuwa album yake itakuwa TIDAL tu “My album will never never never be on Apple,” he tweeted at the time. “And it will never be for sale… You can only get it on Tidal.” Kanye na TIDAL wamepata faida ya zaidi ya dola milioni $84
Kanye ni miongoni mwa watu wanaomiliki TIDAL akiwa na Jay Z, Beyoncé, Madonna, Rihanna, J. Cole, na Nicki Minaj.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes