Latest in Tech

MICHEZO

SIASA

VIDEOS

Latest Updates

Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

Huu ndo ujio mzito na mpya wa Ray C kimuziki

08:03:00





Kutoka Kushoto: Anna Peter wa East Africa Radio, Ray C na Mamy Baby wa Clouds FM

Miaka minne iliyopita, kwa hali aliyokuwa nayo, kila mtu alimkatia tamaa kuwa ndio basi tena ameshatumbukia kwenye shimo waliloshindwa kutoka vijana wengi. Matumizi ya madawa ya kulevya yalimuongezea jina la uteja lililolifunika jina lake la utani ‘kiuno bila mfupa.’ Rehema, msichana mrembo aliyekuwa ndoto ya wanaume wengi, akapoteza thamani yake.
Jina lake likapotea kwenye ramani ya muziki na akawa mtu wa kuonewa huruma. Na kwa jinsi madawa ya kulevya yalivyo, humnyong’onyeza mtumiaji, humpunguzia utimamu wake kiakili, humpa utegemezi unaotesa yasipotumiwa na ikawa wakati mwingi Rehema akawa wa kukutwa amezima! Maskini wa Mungu Ray C akaingia kwenye dimbwi la maji ya moto ya uteja, nani wa kumuokoa?
Kwa alama aliyoiweka kwenye muziki wa Tanzania kwa nyimbo kibao zilizofanya vizuri, Ray C akapata msaada kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa zaidi nchini, Rais Jakaya Kikwete. Alijitolea kumpeleka rehab, kumsadia kwa hali na mali hadi hali yake ikarudi kwenye mstari – walau kwa muda huo. Aliingia kwenye mpango wa kutumia methadone aliodumu nao kwa takriban miaka mitatu.
Katika kipindi hicho, Ray C akageuka kuwa kinara wa vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya. Alianzisha pia taasisi yake, The Ray C Foundation kwaajili ya kampeni za kukemea ubwiaji unga. Katika kipindi hicho, Rehema, alijaribu tena kurejea kwenye muziki kwa kuachia wimbo mmoja ‘Mshum Mshum’, ambao hata hivyo haukufanikiwa kumrudisha pale alipokuwa ameishia.
Haikuwa rahisi kuishinda vita hiyo na mwaka huu alionekana kuweka silaha chini kwa kudaiwa kurejea tena kwenye matumizi ya madawa hayo. Video iliyosambaa mtandaoni akionekana akiwa kwenye mvurugano wa akili, akilia na kutaka kujichoma kisu, ilirejesha tena hofu kwa wapenzi wa muziki kuwa amerudi kwenye jela ya uteja.
RAY C ANARUDI
Peleka mbele hadi wiki moja iliyopita, Ray C anaonekana kupata chaji ya muziki inayompeleka hadi kwenye studio za kisasa za Wanene Entertainment. Kwanza nimefurahi kuona amebadilika mno kutoka yule msichana aliyenenepa hadi kuupoteza utambulisho wake. Amerudisha umbo lake la zamani linalompa matumaini ya kulikomboa jina la jukwaani – kiuno bila mfupa.

Uhakika nimeupata kwenye video alizoziweka Instagram zikimuonesha akiwa kwenye mazoezi makali ya kucheza huku kiuno chake kikifuata vyema maagizo kinayopewa. Huu unaweza kuwa urejeo wenye nguvu zaidi wa muimbaji huyu na namuomba Mungu amsaidie kukaa tena kwenye nafasi yake.
Muziki wa Tanzania unamhitaji Ray C hasa kwakuwa kuna upungufu wa wasanii wakubwa wa kike. Inanipa moyo kuona mahaba yake ya muziki yamerudi kwa kasi ya ajabu. Napata amani nikimuona anavyofurahia mchakato wa kutengeneza nyimbo mpya. Nafarijika kuona kuwa amezungukwa na watu wanaotaka arudi kwenye chati.
Atakachohitaji baada ya hapo ni kuungwa mkono na vituo vyote vya redio nchini na pia mashabiki wakitimiza wajibu wao. Yapaswa kukumbuka kuwa muziki pekee ndio unaweza kuwa mkombozi kwake na unaoweza kumpa nafasi ya pili – nafasi ya kung’ara tena.
Naamini anarekodi nyimbo nyingi na katika hizo lazima kutakuwa na nyimbo kubwa. Pamoja na matatizo yote aliyoyapita, sijawahi kuwa na shaka na kipaji chake. Nasubiri kwa hamu kusikia kile alichotuandalia.

VIDEO: TAZAMA UWEZO WA RAPA HUYU WA KIKE MWENYE UMRI WA MIAKA 13 ALIYESAINI SONY MUSIC

11:27:00
Lebo kubwa ya muziki Epic/Sony records wamefanya usajili mkubwa wiki hii baada ya kupata saini ya rapa Luis Rivera Jr Aka Lil Poopy mwenye miaka 13.

Lil Poopy alikuwa msanii wa French Montana kwenye kundi lake la Coke Boys na kutoa mixtape iliyopewa jina “Coke Aint A Bad Word“.
Album hii ilileta matatizo kwenye familia ya Lil Poopy na baba yake mzazi kuchunguzwa na polisi baada ya mtoto wake mwenye miaka 13 kuimba kuhusu Wanawake, dawa za kulevya ,ngono na magari ya thamani.

Msanii huyu anafananishwa na wasanii kama Bow wow,Lil Romeo na Taylor Swift walioanza muziki wakiwa wadogo.

Hii ndo list ya wasanii wanaotajwa kuwania tuzo za BET Hip-Hop 2016

06:04:00
Tuzo za hiphop za BET ziko njiani na tayari wametangaza wasanii wanaowania tuzo hizi kwenye vipengele tofauti, Kwa miaka mitatu mfululizo Drake ametajwa kuongoza kwenye vipengele vingi zaidi anavyowania msanii yoyote, Drake anawania tuzo kwenye vipengele 14 ambavyo ni kama Album of the Year, Track of the Year,na MVP of the Year.
Msanii Future anawania vipengele 10 ambavyo ni kama Album of the Year, Best Mixtape, na Made-You-Look Award kwa Best Hip-Hop Style.
DJ Khaled anawania vipengele 9 na Kanye West 8.
BET Hip-Hop Awards zinafanyika jumamosi ya  Sept. 17 kwenye ukumbi wa Cobb Energy Performing Arts Centre mjini Atlanta,na kuonekana kwenye tv Oct. 4
Orodha kamili ndio hii ya tuzo za BET Hip-Hop 2016.
Best Hip-Hop Video
2 Chainz – “Watch Out”
Desiigner – “Panda”
DJ Khaled feat. Jay Z & Future – “I Got the Keys”
Drake – “Hotline Bling”
Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared – “All the Way Up”
Kanye West feat. Rihanna – “Famous”
Best Collabo, Duo or Group
DJ Khaled feat. Drake – “For Free”
DJ Khaled feat. Jay Z & Future – “I Got the Keys”
Drake & Future – “Jumpman”
Drake feat. Wizkid & Kyla – “One Dance”
Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared – “All the Way Up”
Best Live Performer
Drake
Future
J. Cole
Kanye West
Kendrick Lamar
Lyricist of the Year
Chance the Rapper
Drake
J. Cole
Kanye West
Kendrick Lamar
Video Director of the Year
Benny Boom
Colin Tilley
Director X
Hype Williams
Kanye West
DJ of the Year
DJ Drama
DJ Envy
DJ Esco
DJ Khaled
DJ Mustard
Producer of the Year
DJ Mustard
Dr. Dre
Metro Boomin
Mike WiLL Made-It
Pharrell Williams
MVP of the Year
DJ Khaled
Drake
Future
Kanye West
Kendrick Lamar
Track of the Year
“All the Way Up” – Produced by Cool & Dre and Edsclusive (Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared)
“Controlla” – Produced by Boi-1da (Drake)
“Hotline Bling” – Produced by Nineteen85 (Drake)
“I Got the Keys” – Produced by Southside (DJ Khaled feat. Jay Z & Future)
“Panda” – Produced by Menace (Desiigner)
Album of the Year
DJ Khaled – I Changed A Lot
Dr. Dre – Compton
Drake – Views
Fetty Wap – Fetty Wap
Future –DS2
Kanye West – The Life of Pablo
Best New Hip-Hop Artist
Anderson .Paak
Bryson Tiller
Chance the Rapper
Desiigner
Tory Lanez
Hustler of the Year
DJ Khaled
Drake
Future
Jay Z
Kanye West
Made-You-Look Award (Best Hip-Hop Style)
A$AP Rocky
Drake
Future
Kanye West
Nicki Minaj
Best Mixtape
Chance the Rapper – Coloring Book
French Montana – Wave Gods (Hosted By Max B)
Future – Purple Reign
Lil Uzi Vert – Lil Uzi Vert Vs. The World
Young Thug – Slime Season 3
Sweet 16: Best Featured Verse
2 Chainz – “No Problem” (Chance the Rapper feat. Lil Wayne & 2 Chainz)
Drake – “Work” (Rihanna feat. Drake)
Kendrick Lamar – “Freedom” (Beyoncé feat. Kendrick Lamar)
Kodak Black – “Lockjaw” (French Montana feat. Kodak Black)
Nicki Minaj – “Down in the DM” – Remix (Yo Gotti feat. Nicki Minaj)
Impact Track
J. Cole – “Love Yourz”
Jay Z – “Spiritual”
Jidenna – “Long Live the Chief”
Raury feat. Key – “Trap Tears”
Sir The Baptist feat. ChuchPeople – “Raise Hell”
People’s Champ Award
Desiigner – “Panda”
DJ Khaled feat. Drake – “For Free”
Fat Joe & Remy Ma feat. French Montana & Infared – “All the Way Up”
O.T. Genasis feat. Young Dolph – “Cut It”
Travis Scott – “Antidote”
Young Thug – “Best Friend”

Picha: alikiba kuachia video kali mpya akiwa na warembo hawa wakali

10:12:00
Alikiba yuko mbioni kuachia silaha yake mpya. Staa huyo wa ‘Aje’ ameonjesha kidogo kile kitakachoonekana kwenye video ya ngoma yake mpya, na mashallah itakuwa na warembo haswaaa.Staa huyo ameshare picha akiwa mbele ya jumba la kifahari na warembo wanane jijini Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa huko mwezi uliopita.
Pia ameshare video akiwa na video queen aitwaye, Michaela Roy.

Fiesta Mwanza kumdondosha Wizkid

07:25:00

Clouds FM wamethibitisha kumdondosha hitmaker huyo wa ‘Shabba’ Jumamosi, August 20.


“Kituuuuuuu #DealDone kwa mara ya kwanza ndani ya Mwanza #StarBoY wako @wizkidayo utatapata kumshuhudia LIVE juu ya jukwaa la #Fiesta2016 #Imooooo,” wameandika Clouds.
Hii itakuwa mara ya pili muimbaji huyo anakuja Tanzania. Mwezi October mwaka jana alitumbuiza kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Hiki ndicho kiasi cha Pesa alichokuwa akilipwa Hanscana na Wanene Entertainment.

06:57:00
Kama ulikuwa una shauku ya kujua kiasi cha pesa ambacho muongozaji wa video nchini Hanscana alikuwa analipwa na studio za Wanene,uongozi wa studio hizo wametaja kiasi walichokuwa wakimlipa director Hanscana.
Akiongea kwenye kipindi cha funiko base,Gentriez ambaye ni mmoja watu wa ndani wa kampuni hiyo amesema Hascana alikuwa analipwa sjilingi milioni mbili kila mwezi na studio hizo na pia video zote alizokuwa akizifanya pesa zilikuwa zinaingia kwa Hanscana.
Wanene tulikuwa tunamlipa mshahara hata kabla kampuni haijafunguliwa tulikuwa tunamlipa na video alizokuwa akifanya pesa yote ilikuwa inaingia mfuko kwa Hascana kwa hiyo wanene walikuwa wamewekeza kwake lakini baada ya kufungua kampuni ilibidi kwenye kila kazi lazima kuwe na percent ya kampuni..tulikuwa tunamlipa milioni mbili kwa mwezi” alifunguka Gentriez

Rapa Young Thug abadilisha jina lake la kimuziki

06:52:00
Rapa mwenye mikogo tofauti kwenye muziki ,tabia na mavazi yake Young Thug amesema anampango wa kubadilisha jina lake na kujiita  ‘No, My Name Is Jeffery
Young Thug anategemewa kutangaza jina hili jipya muda wowote sasa kwa mujibu wa mmiliki wa lebo ya 300 ‘Lyor Cohen‘.
Jeffery imetajwa kuwa album mpya ya Young Thug yenye mastaa kama Elton John, Birdman, Swizz Beatz, na Floyd Mayweather.
Jeffery Lamar Williams ndio jina halisi la Young Thug na leo August 16 amefikisha miaka 25.

The Game ajitamba kuwa amelala na dada wote watatu wa Kim Kardashian.

06:46:00
Rapa The Game amejitamba kuwa amelala na dada watatu wa Kim Kardashian ila mpaka sasa hajawataja kwa majina. Kupitia wimbo wake mpya wa “Sauce,” The Game anasema amelala na Kardashians watatu .
Kwenye mtari huu The Game anasema “I used to f*** bhes that Usher Raymond passed off / Then I fed three Kardashians – hold that thought.
Kwenye wimbo huu “Sauce” into iliyotumika ni ya Dj Khaled na mwisho wa wimbo anasema “I got 99 problems, but the sauce ain’t one.” Game yupo studio akifanya album yake ya 1992,

BEEF LAMFAIDISHA MEEK MILL

06:13:00
Msanii wa lebo ya Rick Ross ‘Maybach Music Group’ Meek Mill ambaye kwa sasa yupo kwenye beef na rapa Drake amefanikiwa kufikisha kopi milioni moja ya mauzo kwenye wimbo aliofanya na hasimu wake huyo.
Collabo ya Meek Mill na Drake “R.I.C.O.” imefikisha mauzo milioni moja na kutangazwa kuwa Platnum Single. Wimbo huu ulitoka mwaka 2015
Hivi karibuni mtu wa karibu na mwalimu wa muziki wa Drake ‘Jas Prince’ alisema beef ya Drake na Meek inakaribia kuisha.

Ray J amkana binti ye OBAMA

06:07:00
Rnb staa Ray J ametoa maelezo juu ya tuhuma zinazomkabili za kumtongoza mtoto wa rais Barack Obama kwenye Dm ya IG.
Staa wa muziki kutoka Marekani Ray J amefunguka juu ya tetesi kuwa amemtongoza mtoto wa rais Barack Obama ‘Malia Obama‘.
Ray J ameweka video online akisema “Sijapenda kinachoongelewa kuhusu mimi,niko nyumbani na familia yangu nasikia eti nimemtafuta mtoto wa Obama kwenye Dm yake, kwanini kila siku mnataka kunishusha, niko positive sana kwenye maish yangu, nategeme kufunga ndoa ijumaa hii sina time na mambo hayo“.
Msemaji wa Ray J naye alisema Ray anategemea kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Princess Love

Rapa aliyekuwa G Unit Young Buck ahukumiwa kwenda jela miezi saba.

03:19:00
Rapa aliyekuwa kwenye kundi la G Unit kabla halijasambaratika amehukumiwa kwenda jela miezi saba.
Young Buck ’35’ jumatano hii amekiri mbele ya mahakama kuvunja masharti ya kifungo cha nje chini ya uangalizi wa polisi na kuhukumiwa kurudi jela miezi saba.
Kupitia Instagram Buck aliomba marafiki zake wawe karibu na yeye akiwa jela
Young Buck alianza kuishi maisha chini ya uangalizi wa polisi toka mwaka 2013 na hapa kati amekuwa akivunja masharti ya kifungo cha nje kwa kukutwa akiwa ametumia marijuana kwenye vipimo vya mkojo na makosa tofauti ya fujo.

Rihanna apata shavu kubwa la kuigiza kwenye filamu ya ‘Ocean Eight’

03:15:00
Staa wa rnb kutoka Marekani Rihanna amepata shavu kubwa sana la kuigiza kwenye filamu ya Ocean Eight, ikiwa inahusu toleo la wanawake.
Rihanna ataigiza na wasanii kama Anne Hathaway, Sandra Bullock, Cate Blanchett, Helena Bonham Carter, Mindy Kaling, na Nora Lum aka Awkwafina).
Filamu itaongozwa na Gary Ross aliyeongoza filamu kama The Hunger Games na itatayarishwa na Steven Soderbergh. Filamu inaanza kurekodiwa October mwaka huu.
Soderbergh aliongoza utayarishaji wa filamu za Ocean toka mwaka 2001 Ocean Eleven,2004 na Ocean Twelve,na 2007 Ocean Thirteen. Mpaka sasa filamu hizi zimetengeneza dola za kimarekani bilioni $1.12 zikiwa na mastaa kama George Clooney, Brad Pitt, Matt Damon, Don Cheadle, na Bernie Mac.
Ukiacha filamu hio RiRi ataonekana kwenye filamu ya Luc Besson Valerian and the City of a Thousand Planets mwaka ujao akiwa na mastaa Cara Delevingne, Ethan Hawke, John Goodman, Clive Owen.Kwenye filamu tulimuona Rihanna kwenye Battleship mwaka 2012 na mwaka 2015 kwenye Home.

VIDEO: CHIDI BENZ AFUNIKA KATIKA INTERVIEW

13:21:00

DIRECTOR HANSCANA AIKACHA WANENE

10:40:00
Muongozaji wa video Tanzania,Hascana amefunguka kuhusu tetesi zilizoenea kwamba amefukuzwa kazi kwenye studio za Wanene entertainment ambazo zilikuwa zinamsimamia katika kazi zake za uongozaji wa video.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo,Hascana amesema kuwa yeye hajafukuzwa na studio hizo bali yeye ndiye amevunja mkataba wa kufanya kazi na studio hizo na kuamua kujitegemea baada ya kuona tayari ameshafanya studio hizo zijulikane ambapo ndio ilikuwa kazi yake kubwa.
Wanene hawawezi kunifukuza kazi” alisema Hanscana, “ni kweli kwa sasa sifanyi kazi na Wanene,jukumu langu likuwa ni kufanya watu waifahamu wanene,kwa kuwa tayari imeshafahamika,jukumu langu nimeshakamilisha” aliongeza Hascana na kusema,”Nimeamua wakati huu kusimama Hascana kama Hascana lakini hatuna ugomvi wowote” na kuongeza kuwa mkataba wake ulitakiwa uishe mwakani lakini ameusitissha baada ya kuona studio hizo zina uwezo wa kusiamama peke yake.

WOLPER KUJA KIVINGINE KIMITINDO

06:32:00
Jacqueline Wolper amesema anakuja na mradi mkubwa wa fashion huku akidai kuwa ndio kitu anachokipenda zaidi katika maisha yake.
Wolper
Amedai kuwa kwa sasa yupo kwenye ujenzi mkubwa wa ofisi yake maeneo ya Kinondoni na kwamba akimaliza ataeleza nini hasa anachofungua.
“Sasa hivi nipo kwenye hatua za mwisho, nipo kwenye tiles ndio namalizia kuweka, nikimaliza pale ndio nitawaambia watanzania, mashabiki wangu na wanaopenda kupendeza ni kitu gani nafanya,” ameiambia Bongo5.
Amedai kuwa hiyo ni sababu kubwa imemfanya apumzike kwa muda kwenye filamu kwasababu suala la usambazaji limegeuka kuwa na changamoto.

Bifu lazuka kati ya The Rock na Vin Diesel kwenye utengenezaji wa Fast 8

06:19:00
Wiki hii The Rock aliwashtua mashabiki wake kwa kuandika kwenye Instagram kuwa baadhi ya waigizaji wenzake wa kiume kwenye filamu ya Fast 8 wana mambo ya kipuuzi.


Haikujulikana hasa alimlenga nani na sasa imebainika kuwa mbaya wake ni muigizaji mkuu wa filamu hiyo, Vin Diesel ambaye pia ni producer.
Inasemekana kuwa jitihada za kuwapatanisha wawili hao zinafanyika. Mara ya mwisho wawili hao walizichapa vikali kwenye filamu hiyo na sasa ugomvi huo umeingia kwenye maisha ya kweli, kwa mujibu wa TMZ.
Uadui huo unaweza kuwa hatari kwa filamu hiyo.
Jumatatu hii, The Rock aliandika ujumbe wa hasira kwenye Instagram akisema:
This is my final week of shooting #FastAndFurious8. There’s no other franchise that gets my blood boiling more than this one. An incredible hard working crew. UNIVERSAL has been great partners as well. My female co-stars are always amazing and I love ’em. My male co-stars however are a different story. Some conduct themselves as stand up men and true professionals, while others don’t. The ones that don’t are too chicken shit to do anything about it anyway. Candy asses. When you watch this movie next April and it seems like I’m not acting in some of these scenes and my blood is legit boiling – you’re right.
Bottom line is it’ll play great for the movie and fits this Hobbs character that’s embedded in my DNA extremely well. The producer in me is happy about this part😉. Final week on FAST 8 and I’ll finish strong.
#IcemanCometh #F8 #ZeroToleranceForCandyAsses
“The Rock’s rant about unprofessional male co-stars was targeted at Vin Diesel,” waliandika TMZ.
Tovuti hiyo imeripoti kuwa wawili hao walikuwa na mkutano wa siri Jumanne hii kujaribu kuyamaliza. Inasemekana kuwa wawili hao walikorofishana kutokana na Vin ambaye ni producer pia kuchukua maamuzi ambayo The Rock hakukubaliana nayo.
“Our sources say The Rock and Vin had a meeting on the Atlanta set mid-day Tuesday … partly because tensions were running so high it was almost impossible to shoot scenes. We do not know if they resolved their issues,” wameandika TMZ.
TMZ awali waliripoti kuwa waigizaji wengi wa filamu hiyo walichukizwa na ujumbe wa The Rock kwakuwa iliwafanya wote wakisiwe wamelengwa.
Chanzo kimoja pia kimeiambia E! News kuwa utengenezaji wa Fast 8 umekuwa mgumu hasa kwa The Rock.
“Things on set just ‘didn’t feel exactly the same’ this time around. And while Johnson ‘is the best guy on the planet to work with,’ he’s ‘also a very emotional guy’ and ‘likes things to go as he sees fit [while] also being fair,’” kilisema chanzo hicho.

50 CENT ATISHIA KUMUUA DIRECTOR WA FILAMU BAADA YA KUUONYESHA UUME WAKE LIVE

06:10:00
50 Cent amevuliwa nguo kwenye tamthilia ya Power baada ya uume wake kuonekana kwenye episode mpya na amechukia.
Katika kile ambacho wengi wanaamini kuwa rapper huyo hakuwa serious, amemwakia mtengezaji wa tamthilia hiyo, Courtney Kemp Agboh kuwa atamuua kwa kuacha uume wake uonekane.
50 na Courtney Kemp Agboh

Rapper huyo anayeigiza kama Kanan kwenye show hiyo alitumia Instagram kuandika: ‘Man I just saw episode 4, of POWER… Courtney I’m a kill you, this is not funny. ‘I think I just saw my (eggplant icon) in a scene. What the f*** Courtney call my phone NOW!!!’
Baadaye aliandika: Auntie G money, 😆 just called me and said man what the fuck did i just watch 😳 she’s traumatized. She said she had to get up twice.”

BILL NAS AKANUSHA KUMCOPY ZILLA

04:34:00
Msanii wa rap nchini,Bill Nas ambaye amekuwa akifananishwa na Godzilla kutokana na style yake ya kuchana amefunguka na kusema kuwa haoni kama style yake ya kuchana inafanana na ile ya Godzilla.
Akihojiwa kwenye kipindi cha The Base cha ITV, Bill Nas amedai kuwa yeye amekuja na muziki wake wa tofauti ambao mwanzo haukwepo kwenye tasnia na yeye haoni kama anamuiga mtu yeyote.
Mimi nimekuja na style yangu,hata ukiangalia nyimbo zangu zina taste ya tofauti.Sioni sehemu ambapo mimi ninafanana na Godzilla labda kwa vile yeye ana rap na kuimba na mimi nina rap na kuimba hivyo ndio vitu tunafanana” alifunguka Bill Nas anayetamba na kibao chake cha Chafu Pozi.

LINAH AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA RAPPER BILLNAS

02:11:00
Kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusiana na ukaribu uliopo kati ya msanii wa bongo fleva,Linah Sanga na rapper Bill Nas ambapo watu wengi wanadai kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi.
Lakini Linah alipoulizwa kuhusiana na tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Bill Nas alikana na kudai kuwa yeye na rapper huyo anayetamba na kibao cha Chafu Pozi hawana mahusiano yoyote ya kimapenzi bali ni rafiki yake wa karibu sana kiasi cha kushirikishana hata siri zao.
Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na Bill Nas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana, sasa hivi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake ndiyo siri yangu, Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa ‘connection’ na ‘Producer’ T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki wangu na ndiyo nikafanya hivyo” alisema Linah kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio

DRAKE AMEAMBIWA ASIJIFANANISHE NA KENDRICK LAMAR

15:55:00
Dj mkubwa wa Marekani anayefanya kazi kwenye radio ya Hot 97 Dj Funkmaster Flex anaonekana kushinda beef kati yake na Drake.

Akiwa kwenye show yake rapa Drake amefunguka huko Ibiza nakusema hamuogopi FunkFlex. Mwaka jana Flex alichochea beef ya Drake na Meek Mill kuhusu Drake kutoandika mashairi yake mwenyewe.

Funkmaster Flex amesikika kwneye mtandao wa TMZ akisema “Nadhani Drake bado anahasira na mimi ila mimi namuheshimu sana ila pia asijiweke sawa na Kendrick Lamar,hawako kwenye ligi moja”
 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes