Latest in Tech

Makubaliano ya amani hatarini Sudan Kusin

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar
Makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini yapo hatarini baada ya kiongozi wa waasi Riek Machar kushindwa kurudi katika mji mkuu wa Juba, wapatanishi wameonya.

Alitarajiwa kuwasili siku ya Jumatatu kuchukua wadhfa wa makamu wa rais katika serikali mpya ya muungano.

Ni swala muhimu katika makubaliano hayo linalolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili.

Marekani imesema kuwa imesikitishwa na hatua ya Machar kushindwa kuafikia ahadi yake.

Upande wa Machar unasema kuwa kuchelewa kuingia kwa Machar kumesababishwa na mipango na maswala mengine ya usimamizi na kwamba alipanga kurudi siku ya Jumatano.

Taarifa kutoka kwa serikali siku ya Jumanne ilisema kuwa kurudi kwa Machar kulicheleweshwa kwa sababu alitaka kuingia na vifaa vikali vya kijeshi.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes