![]() |
| ANC yamtuhumu Malema kwa uhaini |
Chama tawala nchini Afrika Kusini
ANC kimemtuhumu kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom
Fighters (EFF),Julius Malema kwa uhaini.
''Tunaiomba serikali ichukue hatua kali zaidi dhidi ya matamshi hayo ilikuzuia visa vya utovu wa usalama''
Katika mahojiano ya moja kwa moja na shirika la habari la Al Jazeera, bw Malema, alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa 2014 katika jimbo la Gauteng hayakuwa ya haki na akaonya dhidi ya wizi wa kura katika uchaguzi ujao wa kimkoa.
''Sehemu moja ya wajibu wetu wa mapinduzi ni kupigana na iwapo itatubidi ,hatutakuwa na ila bali kuchukua silaha na kutetea haki zetu.Tutapigana. alisema bw Malema.
Chama tawala cha ANC kinamtuhumu Malema kwa kukiuka kanuni za kitaifa za uchaguzi kwa kuwachochea watu wapigane.
Kodwa alisema kuwa hiyo ni kinyume cha sheria ya nchi.


Post a Comment