Latest in Tech

rais zuma atua Iran leo

jacob zuma
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini yuko nchini Iran kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Zuma ameandamana na ujumbe mkubwa wa maafisa wa serikali na wafanya biashara.

Mazungumzo yanatarajiwa kuhusu kujenga tena uhusiano wa kibiashara, ambao ulikatwa wakati Iran ilipowekewa vikwazo vya kimataifa, kwa sababu ya mradi wake wa nyuklia.

Rais Zuma alisema baada ya vikwazo hivyo kuondoshwa, fursa mpya zimefunguka, za kufanya biashara baina ya Iran na bara la Afrika.

Bidhaa ambazo Afrika Kusini iliiuzia Iran mwaka wa 2014, zilikuwa asili mia 20 tu ya kiwango cha miaka sita iliyopita.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes