Latest in Tech

SPURS YAUPUNGUZIA KAZI LEICESTER


Spurs wamo alama saba nyuma ya Leicester
Klabu ya Leicester City itashinda Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili iwapo itafanikiwa kulaza miamba Manchester United uwanjani Old Trafford Jumapili.

Ushindi nyumbani kwa mabingwa hao mara 20 wa Uingereza utatosha kuwahakikishia taji baada ya Tottenham kutoka sare 1-1 na West Brom Jumatatu.

Mabao yote mawili yalifungwa na beki wa West Brom Craig Dawson, moja la kujifunga dakika ya 33 lakini baadaye alifidia kwa kufunga dakika ya 73.

Matokeo hayo yaliwaacha Spurs wakiwa alama saba nyuma ya Leicester, kila timu ikiwa imesalia na mechi tatu za kucheza.

Leicester City, chini ya meneja Claudio Ranieri, walianza msimu uwezekano wao wa kushinda ligi ukiwa 5,000-1.
Lakini Arsenal, Manchester City, Manchester United na mabingwa watetezi Chelsea, ambao kawaida ndio hupigania taji, wameshindwa kufana msimu huu.

Akiongea baada ya mechi hiyo ya Jumatatu, meneja wa West Brom Tony Pulis aliambia BBC Radio 5 kwamba: "Ninataka Leicester washinde. Leicester wana hadithi ya kusisimua na sidhani inaweza ikajirudia kwengineko ila hapa kwetu nchini.


Leicester wameshangaza wengi msimu huu
"Kile Leicester wanaweza kufanya ni kujikakamua na kupata matokeo mazuri kama walivyofanya. Nafikiri ni jambo la kusisimua. Lakini bado wana kibarua kigumu.”
Leicester, wanaomilikiwa na tajiri Vichai Srivaddhanaprabha kutoka Thailand, hawajawahi kushinda Ligi ya Premia katika historia yao ya miaka yao 132.

Tayari wamefuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara yao ya kwanza kabisa.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes