![]() |
| Mashabiki na wachezaji wa timu ya Kenya |
Biashara zote zilisimama katika
uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya huku shangwe na nderemo
zikitawala eneo hilo siku ya Jumanne wakati timu ya mchezo wa raga ya
Kenya ya wachezaji saba kila upande ilipowasili baada ya ushindi wake
huko Singapore.
You need to install Flash Player to play this content.
Miongoni mwa wale walioilaki timu hiyo ni pamoja na waziri wa michezo Hassan Wario na Mwenyekiti wa muungano wa wachezaji wa raga Richard Omwela.
Ni mara ya kwanza kwa Kenya kushinda taji hilo katika msururu wa mashindano ya 7s duniani baada ya kufika fainali mara mbili mjini Adelaide 2009 na Wellington 2013.



Post a Comment