Afisa wa usalama wa Marekani
amempiga risasi na kumjeruhi mwanamume mmoja aliyeonekana amebeba
bunduki nje ya Ikulu ya White House.
Maafisa wa Usalama wamesema
kuwa mtu huyo alielekea kwenye mojawapo wa milango ya kuingia katika
Ikulu huku amebeba silaha hiyo. Alipoamriwa aiweke chini silaha hiyo
chini akakaidi. Watu walizuiliwa kukaribia Ikulu hiyo ya White House
kwa muda, huku maafisa wa Usalama wakikimbia kuhakikisha kuwa Makamu wa
Rais Joe Biden, aliyekuwa katika jengo hilo wakati huo, alikuwa salama.
Rais Obama alikuwa ameondoka kwenda kucheza mpira wa gofu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa walisikia mlio wa risasi na kisha wakamwona mwanamume mmoja mzungu akianguka chini.
Post a Comment