![]() |
| Joaquin Guzman, almaarufu El Chapo alikamatwa mwezi Januari. |
Mexico imeidhinisha
kuhamishiwa Marekani mlangunzi mkuu wa madawa ya kulevya, Joaquin
Guzman, almaarufu El Chapo, ili ashtakiwe kwa mauaji na ulanguzi wa
madawa ya kulevya.
Mawakili wa Guzman wamesema kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
El Chapo, aliyesimamia kundi la walanguzi wa madawa ya kulevya lijulikanalo kama Sinaloa alikamatwa Januari, miezi sita baada ya kutoroka kutoka gereza moja la Ulinzi Mkali kwa kuchimba mtaro chini ya ardhi hadi katika seli yake.


Post a Comment