Mgombea mkuu wa chama cha Republican Donald Trump ameshutumu Uchina na
kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani kupitia sera zake za kibiashara.
Ameambia watu waliohudhuria mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina
imekuwa ikitekeleza “wizi mkubwa zaidi kuwani kutekelezwa katika
historia ya dunia.”
Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, amekuwa akiituhumu
Uchina kwa kuchezea sarafu yake ili kuwa na ushindani wa kibiashara
duniani inapouza bidhaa nje ya nchi.
Hilo, amesema, limeathiri sana wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani.
“Hatuwezi kuruhusu Uchina iendelee kuibaka nchi yetu, na hilo ndilo tunafanya (kwa wakati huu),” alisema mkutanoni Jumapili.
"Tutabadilisha mambo, na tuna uwezo, msisahau. Tuna nguvu sana dhidi ya Uchina.”
Katika manifesto yake ya kampeni, Bw Trump ameahidi kufanikisha mkataba
bora wa kibiashara baina ya Uchina na Marekani ambao utawezesha
“wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka Marekani kuweza kushindana”.
Obama: Trump haelewi sera za kigeni
Ametaja malengo manne ambayo yanahusisha kutangaza Uchina kuwa taifa
linalochezea sarafu yake na kusitisha utoaji wa nafuu za wafanyabiashara
wanaouza bidhaa nje ya nchi ambazo anasema ni haramu.
Aidha, anaitaka Uchina kufikisha kikomo mfumo duni wa masharti ya leba na uhifadhi wa mazingira.
Takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa serikali ya Marekani zinaonesha
pengo la kibiashara baina ya Uchina na Marekani lilipanda na kufikia
$365.7bn (£250.1bn) mwaka jana. Kufikia Februari mwaka huu, pengo hilo
lilikuwa limefika $57bn tayari.
Hii ni mara ya kwanza kwa Trump kutumia neno “ubakaji” akizungumzia
biashara na Uchina, lakini amejulikana kwa kutumia maneno makali kwenye
kampeni yake.
Alikabiliwa na mamia ya waandamanaji jimbo la California Ijumaa kabla
yake kutoa hotuba katika mkutano wa chama cha Republican Ijumaa.
Alilazimika kutumia mlango wa nyuma kuingia.
Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang amesema Wachina wanafuatilia kwa karibu uchaguzi nchini Marekani.
Hata hivyo anasema wengi wanamtazama Bw Trump kama mtu wa kuenziwa badala ya adui.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment