![]() |
| Clinton anahitaji wajumbe 90 kupata ushindi |
Mgombea urais anayeongoza katika
chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton amesema haiwezekani
iwe kwamba hatakuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Novemba.
"Nitakuwa mgombea wa chama change,” ameambia CNN.
“Hilo limekamilika tayari, kimsingi. Haiwezekani hilo lisitokee.”
Bi Clinton ana idadi kubwa ya wajumbe, wajumbe 2,293 na anahitaji wajumbe 90 pekee kujihakikishia ushindi.
- Trump: Ninaweza kuzungumza na Kim Jong-un
- Trump alegeza msimamo kuhusu Waislamu
- US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
Lakini maafisa wa Sanders wanasema Bi Clinton hafai kudhani kwamba tayari ameshinda, wakitaja ushindi wa karibuni wa Bw Sanders katika majimbo ya Indiana, West Virginia na Oregon.
Amesema mfanyabiashara huyo tajiri kutoka Marekani ni hatari kwa demokrasia Marekani na kwamba msimamo wake kuhusu sera ya kigeni ni hatari sana.


Post a Comment