![]() |
| Roger Federer ajitoa katika mashindano kwa ugonjwa |
Roger Federer amejiengua katika
mshindano ya wazi ya Ufaransa mwaka huu baada ya kushindwa kupona
maumivu ya mgongo yanayomkabili.
Alirejea katika mashindano ya wazi ya Italia lakini aliondolewa kwenye raundi ya tatu na Dominic Thiem.
''Ninaendelea vizuri lakini sio kwa asilimia 100,''alisema mchezaji hi=uyo namba tatu kwa viwango vya mchezo huo duniani. ''Nafikiri naweza kujiweka pabaya kama nitacheza katika mashindano yoyote bila kupona vizuri''. ''Maamuzi haya hayakuwa mepesi kufanya,lakini niliamua kuacha kucheza ili pia nipumzike vyema''
Hii inamaanisha kuwa Federer atakosa kucheza Grand Slam kwa mara ya kwanza ndani ya karne hii.


Post a Comment