Jacqueline Wolper anaweza kuwa kimya kwenye filamu kwa kipindi kirefu lakini ana mipango mikubwa kwenye tasnia hiyo.
Muigizaji huyo amedai kuwa na mpango wa kuja na filamu
aliyoshirikiana na ex wake Diamond Platnumz. Wolper ambaye kwa sasa ni
mpenzi wake na Harmonize, alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV
wiki hii kuwa pamoja na kwamba aliwahi kuwa na uhusiano na staa huyo na
kisha kuachana, bado wamebaki kuwa washkaji wa nguvu.
Alisema ukaribu wao ni zaidi ya urafiki na wameendelea kushirikiana
katika mengi. Ni kweli kwakuwa Wolper ndiye ex wa Diamond pekee
aliyeonekana kwenye video ya Utanipenda.
Hata hivyo hakusema ni lini filamu hiyo itaanza kufanyiwa maandalizi. Kama itakuwepo, hiyo itakuwa filamu ya kwanza ya Diamond.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment