![]() |
| Kim amesifu mpango wa nyuklia wa taifa hilo |
Mkutano mkubwa wa chama tawala
nchini Korea Kaskazini umeanza huku Rais Kim Jong Un akisifu hatua
zilizopigwa na taifa hilo katika kuunda silaha za nyuklia.
Bw Kim amehutubia maelfu ya wajumbe, waliokusanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Pyongyang.
Anatarajiwa kutia nguvu utawala wake wakati wa mkutano huo.
Wachanganuzi wa mambo wanatarajia pia kwamba atatangaza mpango kuhusu mageuzi ya kiuchumi huku akisisitiza azma ya taifa hilo ya kuendeleza silaha zake za nyuklia.
Kuna matarajio kwamba huenda jaribio la tano la bomu la nyuklia likafanyika wakati wa mkutano huo.
Wanahabari 100 kutoka nchi za nje wamealikwa kuangazia mkutano huo.
Hakuna mkutano mkuu wa chama uliofanyika wakati wa utawala wa babake Kim Jong-un, Kim Jong-il aliyefariki mwaka 2011.
Wakati wa mkutano wa mwaka 1980, uliofanyika kabla ya kuzaliwa kwa Kim Jong-un, ndipo Kim Jong-il alipotambulishwa kama mrithi wa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung.
Licha ya kifo chake 1994, Kim Il-sung, aliyetawazwa kuwa “rais wa milele, kirasmi bado ndiye kiongozi wa mkutano huo mkuu wa chama ambao unatarajiwa kudumu siku kadha.



Post a Comment