![]() |
| Rolling Stones |
Wanamuziki wa The Rolling Stones
wamemtaka mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Demokrat Donald
Trump kuwacha kucheza muziki wao wakati wa kampeni zake za urais.
Bendi ya Rolling Stones haijatoa ruhusa kwa kampeni ya Trump kutumia nyimbo zao na sasa inaitaka kampeni hiyo kukoma kutumia muziki wake mara moja.
Mgombea huyo amekuwa akicheza nyimbo hizo katika mikutano yake ya kampeni kwa miezi kadhaa sasa.Kibao chao kilichovuma mwaka 1969 ''You Cant Always Get What You Want'' kimekuwa maarufu.
Mnamo mwezi Februari ,Adele alitoa taarifa akijiondoa katika uhusiano wowote na Trump baada ya kucheza muziki wa nyota huyo ''In The Deep'' katika mikutano yake.
Mwanamuziki huyo alitoa taarifa akiweka wazi kwamba hajampatia ruhusa mgombea huyo kutumia muziki wake kwa kampeni zake za kisiasa



Post a Comment