Jurgen Klopp amefanikiwa kuifikisha
Liverpool katika hatua ya fainali ya ligi ya Uropa baada ya kuibuka na
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal.
Baada ya mchezaji wa Villareal Victor Ruiz kutolewa kwa kadi nyekundu, Adam Lallana alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu usiku wa Alhamisi na kufanya mambo kuwa 3-0.
Klopp ambaye alichukua timu hiyo kutoka kwa Brendan Rodgers mwezi Oktoba mwaka jana ameshaifikisha Liverpool katika fainali mbili huku ya kwanza ikiwa katika kombe la ligi ambapo walipoteza dhidi ya Manchester City. Kwa matokeo hayo watakutana katika fainali na mabingwa watetezi Sevilla mjini Basel Mei 18.
Sevilla walifika fainali kwa kuwacharaza Shakhtar Donetsk kwa matokeo ya jumla ya 5-3.


Post a Comment