Marekani inasema kuwa inashughulikia
mipango fulani ili kuzuia kulipuka upya kwa mapigano nchini Syria na
kufufua usitishwaji wa maovu kote nchini humo.
Marekani imekuwa ikiishawishi Urusi ikiitaka iishinikize serikali ya Syria kuachana na kile inachosema kuwa mashambulizi ya kiholela .
Hata hivyo Urusi inasisitiza kuwa mashambulizi ya mjini Allepo ni sehemu mapigano dhidi ya makundi ya kigaidi.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani John Kerry leo Jumapili atakuwa mjini Geneva kuzungumzia hali ilivyo pamoja na mjumbe maalum ya umoja wa mataifa nchini Syria Staffan de Mistura pamoja na mawaziri wa kigeni wa Jordan na Saudi Arabia.
Post a Comment