Aliyekuwa mchezaji nambari moja wa
tenisi kwa upande wa wanawake Maria Sharapova huenda asicheze tena baada
ya kubainika kwamba amekuwa akitumia dawa za kusisimua misuli, rais wa
shirikisho la mchezo wa tenisi nchini Urusi amesema.
Alipoulizwa iwapo Sharapova atashiriki katika michuano mengine,Shamil Tarpishchev aliambia kitengo cha habari cha R-Sport kwamba hadhani, akiongezea kwamba mshindi huyo mara tano wa Grand Slam alikuwa katika hali mbaya.
Mnamo mwezi Machi,Sharapova alisema kuwa alikuwa tayari kuendelea na tenisi.
Shirikisho la kimataifa la mchezo wa tenisi ITF lilimpiga marufuku kwa mda Sharapova mnamo tarehe 12 mwezi Machi.
Anasubiri kusikia adhabu yake kamili ,ambayo huenda ikawa marufuku ya miaka minne,ijapokuwa wataalam wanasema huenda akapewa marufuku ya miezi sita au 12.


Post a Comment