![]() |
| Mashabiki wa Liverpool |
Zikiwa zimesalia Saa chache kabla ya
fainali ya kombe la Europa League kati ya Liverpool na Sevilla, polisi
mjini Basel, Uswizi wametoa onyo kutowaruhusu mashabiki wa Liverpool
wasiokuwa na tiketi kuingia au kukaribia uwanja wa St Jakob-Park.
Takriban mashabiki laki moja wanatarajiwa kufika nchini humo kuiandama
timu yao ya The Reds wakisaka ubingwa wa bara Ulaya.
Knuchel ameongeza kuwa, wako tayari kuwapokea mashabiki wa Liverpool na kuwapa mazingira mazuri ya kusherekea.
"Kama huna tiketi ya kutazama mechi, usikaribie uwanja kwa sababu kuna sehemu za ukaguzi na hutoruhusiwa kuingia uwanjani. "
"Hoteli zote hazina nafasi, kama unasaka sehemu ya malazi, hautafanikiwa, utasubiri hadi asubuhi utakapoabiri ndege’’, alisema.
Hata hivyo, licha ya tahadhari, polisi wamesema kuwa watakabiliana na mashabiki kwa utulivu bila vurugu.
Baada ya ushindi wake dhidi ya Villareal, Kocha Jurgenn Klopp, aliwahimiza mashabiki wasiokuwa na tiketi kuandamana nao. Lakini sasa Klopp amewarai mashabiki wasalie makwao, msimamo unaougwa mkono na polisi wa Liverpool.
Kulingana na polisi wa Uswizi, ndege nane zaidi zimekodishwa ili kuwasafirisha mashabiki wa Liverpool kutoka Uingereza hadi Uswizi.
Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA limeshinikizwa kwa kuandaa fainali katika uwanja mdogo ulio na uwezo wa kuwalaki mashabiki 35,000 pekee.
Wafuasi wa Liverpool wametengewa nafasi elfu kumi pekee.


Post a Comment