![]() |
| Matapeli wa you tube |
Wanachama wanne wa kundi lenye utata
la Trollstation katika mtandao wa Youtube wamefungwa jela kutokana na
wizi wa mabavu na utekaji nyara bandia.
Idhaa hiyo ilio na wateja 718,000 imejijengea sifa kwa kutengeza video bandia mjini humo.
Mwanachama wa tano alifungwa mnamo mwezi Machi kufuatia utapeli wa tukio la bomu.
''Utapeli huo huenda waliouona kama wa kawaida,bila kujua kwamba ulikuwa unawapa dhiki raia wa kawaida ambao wanafaa kuendelea na bishara zao bila kuogofywa''.
''Tunatumai kwamba kifungo hicho kitakuwa mfano kwa wale wanaotekeleza vitendo vya utapeli kama hivi ambavyo haviwezi kukubalika kuendelea mjini London'',alisema Robert Short,afisa wa mashtaka katika huduma ya Crown Prosecution Service


Post a Comment