Baada ya kutumia gharama kubwa mwaka 2014 kuinunua Nokia, Microsoft imeamua kuiuza kwa kampuni ya Foxconn kwa dola milioni 350.
Kwenye dili hiyo kampuni tawi la Foxconn, FIH Mobile Ltd. Itakichukua
kiwanda cha simu cha Microsoft kilichopo Vietnam. Microsoft pia
inaigawa brand ya Nokia na mambo mengine.
Hiyo haimaanishi kuwa Microsoft inajiondoa kabisa kwenye utengenezaji wa simu – itaacha tu kutengeneza vifaa vya Nokia.
Katika maelezo yake, Microsoft inasema itaendelea kutengeneza
Windows 10 Mobile na kusupport simu kama Lumia 650, Lumia 950 na Lumia
950 XL, na simu za kampuni rafiki ya OEM za Acer, Alcatel, HP, Trinity
na VAIO.
Hivi karibuni Microsoft ilipunguza wafanyakazi 8,000 kutoka kwenye
idara yake ya simu na kuziachia dola bilioni 7.6 ilizozitumia kwenye
Nokia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


Post a Comment