Latest in Tech

MICHEZO

SIASA

VIDEOS

Latest Updates

Showing posts with label UCHUMI. Show all posts
Showing posts with label UCHUMI. Show all posts

Kuondoka kwa Uingereza kutoka EU kumeathiri uchumi duniani

05:19:00
Mkutano wa mawaziri wa fedha wa mataifa ya G20, umemalizika nchini China, huku onyo likitolewa kuwa, kura ya maoni iliyoifanya Uingereza kujiondoa ndani ya muungano wa mataifa ya Bara Ulaya, imesababisha hatari kubwa zaidi na kuyumbisha uchumi wa Dunia.
Mkutano huo wa G20 umesema kwamba kuna hatari kubwa kuwa, mazungumzo kuhusiana na hatua hiyo ya Uingereza yakaibua uchungu mwingi.
Lakini viongozi hao wakasema kuwa EU imejiandaa ipasavyo kushughulikia tatizo hilo huku wakisema kuwa wana matumaini kubwa kuwa Uingereza sharti iendelee kuwa mshirikamkubwa wa EU.

Ijodo - Trekta zilizoundwa Nigeria

10:13:00
Mataifa mengi barani Afrika yameathirika pakubwa na baa la njaa.
Ima ni kutokana na mabadiliko ya hali ya anga , ukosefu wa pembejeo za kilimo, ama hata ukosefu wa nguvu kazi ya kuendeleza kilimo.
Kutokana na uhaba wa chakula wa mara kwa mara nchini Nigeria , Mhandisi mmoja amebuni na kuzindua trekta iliyoundwa nchini Nigeria.
Mhandisi Timothy Addigi Terfa ameiambia BBC kuwa alizindua trekta hiyo ya bei nafuu kwa sababu ya upungufu wa mashine hiyo barani Afrika na athari yake kwa kilimo nchini Nigeria.
Aidha mhandisi huyo alisema bei ya trekta barani Afrika inakohitajika mno ni ghali mno.
IJODO
Kulingana naye upungufu huo umesababisha wakulima wengi kuendelea kutumia mikono yao kuendeleza kilimo shambani na hivyo kuathiri pakubwa kiwango cha chakula kinachozalishwa.
Image captionKila trekta aliyounda katika karakana yake itauzwa kwa takriban dola elfu 3,500.
Hilo kwa maoni yake linachangia pakubwa uhaba wa chakula nchini humo.
Kila trekta aliyounda katika karakana yake itauzwa kwa takriban dola elfu 3,500.
Trekta hizo za ''made in nigeria'' zinaitwa IJODO.
Tafsiri yake ni Kazi katika kabila la Tiv.

Magufuli: AirTanzania kupaa tena Septemba

10:10:00

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016''.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa
''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa.
Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza.
Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni.
BIASHARA NA RWANDA
Wakati huohuo rais Magufuli aliueleza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Rwanda kuwa China imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge” kwa nia ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya wafanyabiashara.
Image captionMarais Paul Kagame na mwenyeji wake John Magufuli
''Tanzania imeamua kuipatia Rwanda eneo la kujenga bandari kavu kwa ajili ya mizigo ya wafanyabiashara wake na pia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itafungua ofisi mjini Kigali nchini Rwanda ikiwa ni juhudi za kurahisisha na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.''
Juhudi hizo bw Magufuli anasema ni kuwahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa bandari ya Dar es salaam ni salama kwao kupitisha mizigo na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha bandari hiyo na kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili.
Kwa upande wake rais Paul Kagame wa Rwanda alitoa wito kwa ''Tanzania na Rwanda pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana na sekta binafsi katika kutumia fursa nyingi za kibiashara zilizopo baina yake na kuwaletea manufaa wananchi''.

Bei ya mafuta yapanda na kupita dola 50 kwa pipa

02:56:00
Bei ya mafuta imepanda hadi zaidi ya dola 50 kwa pipa kwa mara ya kwanza kabisa mwaka huu mwaka 2016 wakati uzalishaji wa chini na kuongozeka kwa mahitaji ya mafuta vikiendelea kuchangia kupanda kwa bei.

Kupanda kwa bei ya mafuta kunafuatia takwimu za Marekani zinazoonyesha kushuka kwa uzalishaji hasusan kutokana na moto nchini Canada.
Uzalishaji wa mafuta yasiyosafishwa nchini Marekani ulishuka kwa pipa milioni 4.2 hadi pipa milioni 537.1 kwa wiki kwa mujibu wa idara ya nishati nchini humo..
Canada ndiye muuzaji mkubwa zaidi wa mafuta kwa Marekani na moto wa msituni katika mikoa iliyo magharibi, ulisababisha kupungua kwa karibu mapipa milioni moja kwa siku.

Mazungumzo ya hivi majuzi kati ya nchi za Opec na Urusi kuhusu kupunguza uzalishaji wa mafuta yamechangia kupanda kwa bei.

Microsoft yauza kilichobaki Nokia kwa kampuni nyingine

12:53:00
Baada ya kutumia gharama kubwa mwaka 2014 kuinunua Nokia, Microsoft imeamua kuiuza kwa kampuni ya Foxconn kwa dola milioni 350.

Kwenye dili hiyo kampuni tawi la Foxconn, FIH Mobile Ltd. Itakichukua kiwanda cha simu cha Microsoft kilichopo Vietnam. Microsoft pia inaigawa brand ya Nokia na mambo mengine.

Hiyo haimaanishi kuwa Microsoft inajiondoa kabisa kwenye utengenezaji wa simu – itaacha tu kutengeneza vifaa vya Nokia.

Katika maelezo yake, Microsoft inasema itaendelea kutengeneza Windows 10 Mobile na kusupport simu kama Lumia 650, Lumia 950 na Lumia 950 XL, na simu za kampuni rafiki ya OEM za Acer, Alcatel, HP, Trinity na VAIO.

Hivi karibuni Microsoft ilipunguza wafanyakazi 8,000 kutoka kwenye idara yake ya simu na kuziachia dola bilioni 7.6 ilizozitumia kwenye Nokia.

Nokia wapania kuteka soko la Smartphones na simu zao mpya.

06:45:00
Leo kampuni kubwa ya simu ya Nokia imetangaza rasmi kuanza kutengeneza smart phone za kisasa kutoka kwenye kampuni yao itakayotengeneza simu hizo ya Global HMD. Kampuni hii itawasaidia Nokia kuweza kutengeneza na kuuza simu za Android na tablets.

Kumbuka kuwa kampuni ya Microsoft ndio ina haki za kuuza na kutengeneza Nokia handset toka mwaka 2014, na kwa sasa inauza haki hizo kwa kampuni ya Foxconn’s FIH  kwa dola milioni $350 million.

Hili ndio gari la bei rahisi zaidi china.

06:43:00
Hii imetajwa kuwa gari ya bei rahisi zaidi nchini China, gari hii inaitwa Jiangnan TT inatengenezwa na kampuni ya Jiangnan Auto, bei yani ni  20,800 yuan na punguzo lake ni mpaka 5,000 yuan. Kwa mahesabu ya haraka haraka ni kama dola za kimarekani $2,415 ambayo ni milioni tano za Bongo.
Cylinder tatu, mafuta ni 0.8 liter ha 36 horsepower, speed ya 120 kilometers per hour (75 miles). Gearbox is a four-speed manual.
jiangnan-tt-china-1 jiangnan-tt-china-2

Dola milioni 110 zahitajika kusaidia nchi za Afrika

06:01:00
Ukame umesababisha ukosefu wa chakula kwenye nchi za kusini mwa Afrika
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na chama cha msalaba mwekund wametoa ombi la dola milioni 110 kusaidia nchini za kusini mwa Afrika zilizoathirika na ukame.

Takriban watu milioni 31.6 katika eneo hilo hawana chakula cha kuwatosha kutokana na ukosefu wa mvua na uhaba wa maji.

Ombi hilo linatolewa kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa umoja waimataifa, unatarajiwa kuangazia hitaji la kuchukua hatua, kulinda jamii kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

WAFANYA BIASHARA ZA NGONO WAOMBA KUHALALISHIWA BIASHARA HIYO ILI WAWEZE KULIPA KODI

04:03:00
Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.

Wakizungumza na gazeti la Mwananchi, kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.

Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.

“Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini” alisema Rosemary Kazeze.

Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya kunakosesha serikali mapato.

Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.

“Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein

HII NDIO MIJI GHALI ZAIDI BARANI AFRIKA

09:09:00
10) Abuja 
Abuja ni mji mkuu wa Nigeria. Unakadiriwa kuwa na idadi ya watu 979,876. Umejengwa miaka ya 1980. Kuhusu Abuja, siku moja Nelson Mandela alisema, “Kwa nini ujitese kutembelea Ulaya wakati vitu vyote utavikuta hapa.”

9) Conakry
Conakry ni mji mkuu wa nchi ya Guinea. 
8) Bamako 
Bamako ni mji mkuu wa Mali. Unakadiriwa kuwa na takribani watu milioni mbili.

7) Brazzaville 
Huu ni mji mkuu wa Congo. Unakadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni 1.3.

6) Lagos
Lagos ni mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria.

5) Kinshasa
Ni mji wenye zaidi ya watu milioni nne. Ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

4) Libreville
Libreville ni mji mkuu wa Gabon unaokadiriwa kuwa na zaidi ya watu 500,000. 

3) Victoria
Victoria ni mji mkuu wa Ushelisheli. Ni mji ambao Prince William wa Uingereza na mke wake walienda kupumzika baada ya harusi yao. Inasemekana walitumia zaidi ya dola 5,000 kwa usiku mmoja.

2) N’Djamena
N’Djamena ni mji mkuu wa Chad.

1) Luanda
Luanda ni mji mkuu wa Angola. Katika jiji hili, inaarifiwa kuwa kodi yake inakadiriwa kuanzia Yuro 10,000 mpaka Yuro 35,00o. Maisha sio rahisi kabisa katika jiji hili.

JE? UNAIFAHAMU MIJI GHALI NA TAJIRI ZAIDI DUNIANI

09:00:00
Huu ni mji wa Monaco ukitaka kununua luxury property gharama yake ni $ 1 million kwa 16 square meters Monaco hiyo. Yani ukubwa wa uwanja wa tennis kwa $ 1 million, Mji huu unashika number moja dunia kwa gharama hizo.
Hong kong nako kunakaribia na ya Monaco na huko ni $ 1 million unapata square meters 19 tu kwa bei hiyo inashika number 2 kidunia.
London nako wamo usingizi kwa $ 41, 900 mpaka $ 46,300 kwa square meters 23 unaweza kujidai na kukoloma juu kiroho safi.

mambo haya hapo Geneva kunakoaminika kuwa wanene wengi wameufukia umate mate wao jiji hapa, unaweza kujipatia usingizi wako kabambe kabisa kwa $ 29, 300 mpaka $ 32,400 kwa square meters. kwaiyo mwendo wa #3 kwa ghali.

Hapa ni jiji la Paris nisawa na London bei zake zina pigani vishoka tu kwa usawa gharama zake.

Singapore nako wamo gharama za maisha kwa usingizi wako mwenyewe zinaendana na zile za Ulaya...
Hili ndiyo jiji la wasiolala duniani New York City gharama ya usingizi ndani ya jiji hili ni kuanzia $ 21,800 mpaka $24,100 kwa square meters 44. Kwa bei hii unaweza kupata usingizi wenye ukubwa huu na ukajinafasi kibarazani kwako ukiwa umekunja goti.

Hii ni Sydney mjii ni sawa na New York City bei zake ni chavu moja huku unakunja goti huku unakunyua gharama hazipishani saana, Opera House huko ndiyo habari yenyewe.

Huu Haaa za kichina hizo gharama za usingizi Shanghai ni za kichina vile vile maana .....mh...ni $19,000 mwendo wakichina china unagota kwa $21,700 na change unarudishwa kaz hiyo.

JE? WAZIFAHAMU NCHI TAJIRI ZAIDI BARANI AFRIKA

08:54:00
Ukisema uingie mtaani sasa hivi kumuuliza mtu mmojammoja ni nchi ipi tajiri zaidi Afrika huenda ukapata majibu tofauti lakini uhakika wa hilo upo kwenye ripoti mpya iliyofanywa kwa bara la Afrika.
Nigeria ni nchi ambayo Dunia inajua kuhusu mafuta yao, inajulikana pia majina ya matajiri wao kama akina Alhaji Aliko Dangote.. mengine yanayosikika sana kutoka huko ni ishu kama za mashambulio ya Kigaidi, leo imeingia kwenye headlines nyingine.
Utafiti uliofanyika umekuja na majibu tayari, Nigeria ndio nchi inayoongoza kwa utajiri sasahivi ndani ya Afrika… South Africa iko nafasi ya pili alafu zinafuatia nchi nyingine.
Ninayo list ya Top 10 ya nchi zote hapa.
No.1: Nigeria, hii ina sifa nyingine kubwa kuwa nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi Afrika, na pia utajiri wake unatokana sana na uzalishaji wa mafuta.
No.2: South Africa, sehemu kubwa ya Utajiri wao inatokana na uchimbaji wa madini.
No.3: Misri
No.4: Algeria, nao wako kwenye list ya wauzaji wakubwa wa mafuta na gesi.
No.5: Morocco, uwekezaji wao mkubwa uko kwenye Utalii, viwanda vya nguo na Kilimo.
No.6: Sudan.. sio rahisi kukutana na nguo imeandikwa ‘Made in Sudan’, lakini wao ni wauzaji wakubwa sana wa pamba duniani.
No.7: Kenya, biashara yao kubwa ni chai na kahawa.. sikuwahi kujua kumbe hata biashara ya kuuza maua kwenda Ulaya nayo ni biashara inayoingiza pesa nyingi Kenya.
No.8: Angola.. japo walipitia kipindi kigumu cha vita kwa zaidi ya miaka 25, bado madini, mafuta na kilimo vimeiweka nchi hiyo ndani ya Top 10 ya nchi tajiri Afrika.
No.9: Libya.. Hii ndio nchi ya kwanza Afrika ambayo wataalam wamesema kuwa ina akiba kubwa ya mafuta ndani ya Afrika mpaka sasa, na hiyo ndio inayoiingizia nchi hiyo pesa nyingi zaidi kila siku.
No.10: Tunisia.. wao biashara yao kubwa ni spare za magari, kuuza mafuta na utalii.

JE? UNAMFAHAMU KIJANA MTANZANIA TAJIRI ZAIDI BARANI AFRIKA

08:50:00
Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.

Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania .

“Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti hiyo.

Metl ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.

Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.

Kwa mujibu wa tovuti yake, Metl inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.

Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Dewji anashika nafasi mbili juu zaidi ya kada maarufu wa CCM na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Aziz Rostam (50) aliyewekwa nafasi ya mwisho.

Rostam amefungana nafasi ya 26 na mabilionea wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu na Femi Otedola wenye utajiri wa Sh1.8 trilioni kila mmoja.

Orodha hiyo ya 29 bora inaoongozwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote akiwa na utajiri wa Dola 15.7 bilioni za Marekani (Sh28.2 trilioni), kiwango ambacho ni mara moja na nusu ya bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka 2014/15.

Forbes linamtaja Rostam kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.8 trilioni), kiwango ambacho kimebaki pasi na mabadiliko kutoka orodha ya mwaka jana. Rostam anamiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Vodacom.

WAFAHAMU NA KUWAJUA MARASI WANAOONGOZA KWA UTAJIRI AFRIKA

08:46:00
arida la kiuchumi la Forbes limetoa orodha ya viongozi wanane barani Afrika ambao limewataja kuwa ndio wanasiasa matajiri zaidi barani humo. Kwa mujibu wa jarida hilo la Marekani, Rais José Eduardo dos Santos wa Angola anaongoza katika orodha hiyo akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 20 na hivyo kuhesabiwa kuwa, kiongozi tajiri zaidi barani Afrika. Rais do Santos amekuwa madarakani nchini Angola kwa miaka 34 sasa. Wakati rais wa Angola akiongoza kwa kuwa Rais wenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika, asilimia 70 ya wananchi wake wanaishi katika umasikini. Kwa mujibu wa orodha ya jarida hilo la Forbes, Mfalme Muhammad VI wa Morocco anashika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 2.1, Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea anashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo kwa kuwa na utajiri wa dola miloni 600. Aidha kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anashika nafasi ya nne akiwa na utajiri wa dola milioni 500. Wengine walioko katika orodha hiyo ya viongozi wanane matajiri barani Afrika ni Rais Paul Biya wa Cameroon dola milioni 200, Mfalme Mswati III wa Swaziland dola milioni 100, Rais Idriss Deby wa Chad dola milioni 50 na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mwenye utajiri wa dola milioni 10.

WAJUE NA KUWAFAHAMU WATU MATAJIRI ZAIDI TANZANIA

08:30:00
Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka

HAWA NDIO MATAJIRI ZAIDI ULIMWENGUNI

08:23:00

10. Bernard Arnault

  • Net worth : $29 Billion
  • Source : LVMH
Bernard Jean Etienne Arnault is a French businessman and art collector. He had a net worth of $41 USD in 2012 and was fourth richest person in the world. He was born on 5 march 1949 in Roubaix. He joined his father’s company LVMH in 1976 and became CEO in 1977.


9. Liliane Bettencourt

  • Net worth : $30 Billion
  • Source : L’Oreal
Liliane Henriette Charlotte Schueller is a French philanthropist, socialist and businesswomen. In March she was listed in Top wealthiest Women in the World. She is Founder of L’Oreal (one of the largest cosmetic and beauty companies). She is 90.


8. Li Ka-Shing

  • Net worth : $31 Billion
  • Source : Diversified
Li Ka-Shing is the richest person in Asia. He is a Hong-Kong businessman, investor and philanthropist and dropout from school. Born on 13 June 1928. He is currently Chairman ofCheung Kong HoldingsHutchison Whampoa and Li Ka Shing Foundation.

7. Charles Koch

  • Net worth : $34 Billion
  • Source : Diversified
Charles de Ganahl Koch is an American businessman and philanthropist. He was born on 1st November 1935. He is chairman and CEO of Koch industry and one of the top 40 powerful people in the world.


6. David Koc

  • Net worth : $34.5Billion
  • Source : Diversified
David Hamilton Koch is an American businessman , chemical engineer and philanthropist. He was born on 3rd May 1940. He is currently executive vice president of Koch industry and board member of Aspen InstituteCato InstituteReason Foundation.


5. Larry Ellison


  • Net worth : $43 Billion
  • Source : Oracle
Larry Ellison is a self made man and also a college dropout. He is an American businessman , Cofounder and CEO of Oracle corporation. Born on 17 August 1944. In 1970 his company was named relation software inc. And later it is renamed as Oracle.


4. Warren Buffett


  • Net worth : $53 Billion
  • Source : Berkshire Hathaway
Warren Buffett is an American businessman , investor and philanthropist. He was born on 30 August 1930. He is considered as a most successful investor of 20th centurary. He is currently chairman and CEO of Berkshire Hathaway (Self made).


3. Amancio Ortega

  • Net worth : $57 Billion
  • Source : Zara
Amancio Ortega is a Spanish fashion executive. Born on 28 march 1936. He is a founding chairman and CEO of  Inditex fashion group also known as Zara. (Self made). He moves to the world’s top 3 richest person first time.


2. Bill Gates


  • Net worth : $67 Billion
  • Source : Microsoft
Bill Gates is a self made person. His full name is William Henry Bill Gates III and born on 28 October 1955. He is an American businessman , investor, programmer, inventor and philanthropist. He is CEO of the world’s largest software company Microsoft which he cofounded with his friend Paul Allen. He is also Co-Chairman of the Bill & Melinda Gates Foundation, CEO of Cascade Investment Chairman of Corbis and board of members of Berkshire Hathaway. He was the richest person in the world from 1999-2010.
Carlos Slim

  • Net worth : $73 Billion
  • Source : Telcom
Carlos Slim is a Mexican businessman , investor and philanthropist. He is the Richest Person In World since 2010. He is also one of the top 10 most powerful people in the world. Currently he is Chairman and CEO of TelmexAmerica MovilSamsung Mexico and Grupo Carso.
Total Sum up of these Top 10 wealthiest personality is $454.5 Billion.

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes