Latest in Tech

WAFAHAMU NA KUWAJUA MARASI WANAOONGOZA KWA UTAJIRI AFRIKA

arida la kiuchumi la Forbes limetoa orodha ya viongozi wanane barani Afrika ambao limewataja kuwa ndio wanasiasa matajiri zaidi barani humo. Kwa mujibu wa jarida hilo la Marekani, Rais José Eduardo dos Santos wa Angola anaongoza katika orodha hiyo akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 20 na hivyo kuhesabiwa kuwa, kiongozi tajiri zaidi barani Afrika. Rais do Santos amekuwa madarakani nchini Angola kwa miaka 34 sasa. Wakati rais wa Angola akiongoza kwa kuwa Rais wenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika, asilimia 70 ya wananchi wake wanaishi katika umasikini. Kwa mujibu wa orodha ya jarida hilo la Forbes, Mfalme Muhammad VI wa Morocco anashika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 2.1, Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea anashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo kwa kuwa na utajiri wa dola miloni 600. Aidha kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anashika nafasi ya nne akiwa na utajiri wa dola milioni 500. Wengine walioko katika orodha hiyo ya viongozi wanane matajiri barani Afrika ni Rais Paul Biya wa Cameroon dola milioni 200, Mfalme Mswati III wa Swaziland dola milioni 100, Rais Idriss Deby wa Chad dola milioni 50 na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mwenye utajiri wa dola milioni 10.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes