Maelfu ya watu nchini Australia
wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi duniani ya
Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini humo.
Ndege
hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila ya kubeba mzigo
wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito wa tani 117.
Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.


Post a Comment