Mshambulizi chipukizi wa Manchester
United Marcus Rashford ametia sahihi mkataba mpya utakaohakikisha
anasalia Old Trafford hadi Juni 2020.
Rashford ameichezea Man United katika mechi 18 na kuifungia mabao 8.
Rashford amejiunga na timu ya England itakayoshiriki katika michuano ya Euro 2016.
Ijumaa iliyopita talanta yake ilingaa zaidi alipofuma bao la kwanza la kimataifa dhidi ya Australia.
Kijana huyo anakisiwa kuwa analipwa takriban pauni £20,000 kwa Juma.
Naibu mwenyekiti wa Manchester United bwana Ed Woodward alimmiminia sifa kedekede chipukizi huyo
''bado ni kijana sana huyo kwa hivyo tunahitaji kumpa muda zaidi iliakomae kitaaluma , kwa sasa tunashuhudia akinoa makali yake na bila shaka atakuwa mchezaji nyota katika siku za usoni''
Kandarasi hizo zimetangazwa siku 3 tu baada ya kutangazwa kwa kocha mpya Jose Mourinho atakayehudumu Old Trafford kwa kipindi cha miaka mitatu.
Rashford aliwakilishwa na Chris na Wayne Welbeck, ndugu za Danny,anayeichezea klabu pinzani ya Arsenal.


Post a Comment