Watu zaidi ya 60,000 wametakiwa
kuondoka upesi kutoka kwenye mji wa Fort McMurray, Canada kutokana na
moto mkubwa ambao unaendelea kuenea.
Nyumba kadha zimteketezwa na majivu yamekuwa yakianguka katika mji huo wa Fort McMurray.
Wakazi wanaotoroka wamesababisha msongamano mkubwa katika barabara kuu inayotoka mji huo unaopatikana kilomita 380 kaskazini mwa Edmonton.
"Ukitoka tu nje, majivu yanakuangukia. Unaona majivu yakielea angani,” mkazi mmoja aliyetambuliwa kama Mark Durocher amenukuliwa na gazeti la Globe and Mail.
Nyumba katika mitaa miwili zimeteketezwa kabisa na moto huo sasa umesambaa na kufikia barabara ya Highway 63 inayoelekea mji wa Fort McMurray kutoka kusini.
Helikopta inatumiwa kujaribu kudhibiti moto huo.
Kufikia sasa hakujaripotiwa taarifa zozote za majeruhi.


Post a Comment