Watu wanne wametolewa wakiwa hai kutoka kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea ingawa kuna wasiwasi kwamba muda wa kupata manusura wakiwa hai unayoyoma.
Siku mbili zilizopita, mtoto wa umri wa miezi sita aliokolewa baada ya kukaa kwenye vifusi kwa siku nne.
Msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kupelekwa hospitalini.
Babake mtoto huyo, Bw Ralson Wasike, akihutubia wanahabari baadaye, alisema bintiye amekuwa na nguvu sana


Post a Comment