Mchezo huu uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,
ulishudia kikosi cha Yanga, ilipata ushindi wake kupitia kwa magoli ya
mshambuliaji Amisi Tambwe aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya tisa
ya kipindi cha kwanza kisha akaongeza bao la pili katika dakika ya 47
ya kipindi cha pili.
Katika dakika ya 81 winga Deus Kaseke, alihitimisha kazi kwa kufunga bao la tatu baada ya kuunganisha krosi ya Simon Msuva.Bao la kufutia machozi la Azam,liliwekwa kambani na mshambuliaji Didier Kavumbagu.
Licha ya Yanga kushinda mchezo huu wa fainali Azam ndio wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la shirikisho huku Yanga wakiwakilisha katika michuano ya klabu bingwa Africa.

Post a Comment