Latest in Tech

VIDEO: 50 Cent atolewa nduki jukwaani wakati wa show ya T.I na Young Jeezy

Rapa 50 Cent ameshushwa kwenye show ya kituo cha radio cha Hot 107.9 kwenye show uliyokuwa imeandaliwa kwaajili ya T.I. na Young Jezzy. Kwenye hii video 5o Cent anaonekana akilalamika kuwa anashushwa kwenye jukwa hata kabla muda wake haujaisha, ikiwa imebaki dakika moja.
50 Cent akilalamika alisema “Inamaana mnanishusha kwenye jukwa kabla ya muda kuisha, hata dakika moja kweli, sitaki tena mcheze muziki wangu, tuna Youtube.
50 Cent alimaliza kwa kusema ni bora mngenichukia mwaka 2003 kabla sijatoka, kabla sijatoa Get Rich or Die Tryin’ ambayo ilikuwa album ya kwanza ikiwa mpaka sasa imeuza kopi milioni sita. 50 Cent anasema anapesa nyingi sana ila anajidai amepigika tu, ikiwa ni njia za kupunguziwa madeni kitu ambacho anasema hata mgombea urais Donald Trump ameshafanya zaidi ya mara tano.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes