Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limemwita msanii wa muziki wa Hip Hop,
Nay wa Mitego ikiwa ni siku chache toka watangaze kuufungia wimbo wake
‘Pale Kati’ kutokana na wimbo huo kudaiwa kukiuka maadili.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego amesema kwa sasa
hawezi kulizungumzia swala la kufungiwa kwa wimbo wake mpaka pale
atakapofanya kikao na BASATA.
“Kesho nimeitwa BASATA, nadhani itakuwa ni vizuri nikizungumzanao, alafu ndo nije kuzungumza issue ya kufungiwa,” alisema Nay.
Picha ya maandalizi ya video ya pili ya wimbo ‘Pale Kati’ aliyoshoot Afrika Kusini
Hapo awali rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ utakuwa na video
nne tofauti tofauti ambapo mpaka sasa tayari ameshashoot video mbili,
moja akiwa ameshoot Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment