Producer na rapa mkongwe Dr. Dre ametiwa pingu nje ya nyumba yake huko Malibu baada ya tukio la fujo na mtu asiyejulikana lililotokea barabarani.
Mpaka sasa imejulikana tukio hilo lilitokea nje ya nyumba yake na baadae mtu mmoja aliripoti polisi kuwa Dr Dre alimtishia bunduki wakiwa barabarani, ila Dr Dre anasema “Sikumtishia silaha, nilimuomba vizuri tu atoke mbele ya nyumba yangu sababu alizuia mahala napopitisha gari yangu“.
TMZ wameripoti kuwa mwendesha pikipiki huyo alimpigia Dr Dre kelele na baada ya polisi kufika mtu huyo alisema “Here we go again, another black guy with a gun.” akimaanisha “Haya sasa mtu mwingine mweusi akiwa na bunduki”
Hakuna silaha yoyote iliyopatikana kwenye eneo hilo na kwa sasa tunasubiri kujua kama atafunguliwa mashtaka ya kutishia mtu na silaha ya moto
Post a Comment