Matajiri
wa Hispania, Real Madrid wanapanga kumuongezea mkataba wa miaka minne
fowadi wake, Cristiano Ronaldo na kukata mzizi wa fitina juu ya hatima
yake hapo baadaye.
Tangu mwanzoni mwa msimu huu, rais wa klabu
hiyo, Florentino Perez alikuwa na mpango wa kumuachia staa huyo ajiunge
na miamba ya Ufaransa, PSG kwa kitita kilichokadiriwa kufikia euro
milioni 100.
Hata hivyo kitendo cha Ronaldo kufunga mabao zaidi
ya 30 kwa msimu sita mfululizo huku Gareth Bale kipenzi cha Perez ambaye
alitaka awe mbadala wa Ronaldo ameshindwa kuonyesha kiwango pamoja na
kuandamwa na majeruhi.
Licha ya ofa hiyo, huenda kusiwe na
mabadiliko katika mshahara wake wa euro milioni 21 kwa mwaka anazopokea
kwa sasa, zaidi Madrid imenogewa kuendelea naye.
Aidha, kiungo mshambuluaji James Rodriguez na Isco ndiyo wana nafasi kubwa ya kuondoka kwenye majira ya kiangazi.
TAKWIMU ZA RONALDO 2015-16
La Liga
Mechi 34, mabao 31, asisti 11
Ligi ya Mabingwa
Mechi 10, mabao 16, asisti 4
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment