Rais wa Malawi Peter Mutharika,
ametangaza hali ya hatari kutokana na upungufu wa chakula unaosababishwa
na hali ya kiangazi kusini mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa shirika la
habari la AFP.
'Upungufu wa mavuno ya mahindi unatarajiwa kushuka kwa asilimia 12 kutoka kwa mavuno ya mwaka jana,' Bwana Mutharika alisema kupitia taarifa yake.
Watu Zaidi watakosa vyakula vya kutosha na watahitaji misaada mwaka huu wa 2016 na 2017.


Post a Comment