Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin
Mkapa ametangaza kwamba kikao cha kwanza cha mazungumzo ya kutafuta
amani nchini Burundi kitafanyika wiki ijayo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisalia kuwa mpatanishi mkuu.
Mazungumzo ya kutafuta amani yalifeli mwishoni mwa mwaka jana baada ya upande wa serikali kusema hauwezi kuzungumza na watu waliohusika kwa njia moja au nyingine katika jaribio la mapinduzi la mwezi Mei mwaka jana.
Bw Mkapa ameandika kwenye Twitter kwamba wadau wote wanatarajia kuhudhuria kikao cha kwanza cha mazungumzo ambacho kitafanyika mjini Arusha kuanzia tarehe 2 Mei hadi 6 Mei.
"Nimepata idhini kutoka kwa Rais wangu, kiao changu cha kwanza cha Mashauriano ya Burundi kitakuwa mjini Arusha,” aliandika.
Ukosefu wa usalama umeendelea kuwa tatizo kuu nchini Burundi na visa vya watu kuuawa kiholela vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara
Post a Comment