Latest in Tech

Viongozi wa upinzani wakabiliwa na polisi Nairobi



Polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya
Viongozi wa mrengo wa upinzani nchini Kenya (CORD) wamekabiliwa na maafisa wa usalama baada yao kuandamana hadi makao makuu ya Tume ya Uchaguzi (IEBC).

Maafisa wa usalama walianza kushika doria mapema asubuhi jumba la Anniversary Towers, lililo na afisi za IEBC.
Mrengo huo unasema hauna imani na IEBC

Viongozi wa Cord wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni Moses Wetangula walifika mwendo wa saa tano wakiandamana na mamia ya wafuasi lakini maafisa wa usalama wakawazuia kuingia katika afisi hizo.
Bw Wetangula, aliye kiongozi wa chama cha Ford Kenya, ni mmoja wa viongozi walioshiriki

Mrengo huo unataka viongozi wa tume hiyo waondolewa.
Wanasema viongozi hayo hawawezi kutegemewa kuendesha uchaguzi mkuu huru na wa haki mwaka 2017.
Viongozi wa CORD pia wamekuwa wakilalamikia kukataliwa kwa baadhi ya saini zilizowasilishwa na mrengo huo kuunga mkono ombi la kuandaliwa kwa kura ya maamuzi ya marekebisho ya katiba.
IEBC ilisema saini zilizokuwa halali hazikufika saini milioni moja zinazohitajika kikatiba ndipo ombi la marekebisho ya katiba kupitia kura ya maamuzi likubalike.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes