Latest in Tech

OBAMA AVAMIWA NA MASTAA WA MUSIC


Wasanii wakali wa Hip-hop wamepata nafasi ya kutembelea ikulu ya Marekani ‘White House’ na kukutana na rais Barack Obama.
Rais Barack Obama alikutana na wasanii Nicki Minaj, J. Cole, Common, Pusha T, Rick Ross, Chance the Rapper, Ludacris, Busta Rhymes, Alicia Keys, Janelle Monáe, Timbaland na Wale ili kuongelea project ya My Brother’s Keeper.
Nicki Minaj aliandika instagram “Met with President Obama today to discuss a few things that happen to be very dear to my [heart emoji]. I am #MyBrothersKeeper,”
DJ Khaled naye aliandika “I can’t even explain to ya’ll what just happened. History has been made,”
My Brother’s Keeper ilianzishwa na Obama mwaka 2014 ikiwa ni project ya kusaidia vijana wadogo Marekani na dunia nzima kubaki kwenye mstari mzuri wa maisha, kupunguza uovu na tabia mbaya mitaani.
Obama aliongea na rapa Kendrick Lamar kuhusu project hii na iliongelea kwenye video ya Kendrick Lamar ya  “Pay It Forward,”.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes