![]() |
| Add caption |
Taiwan imelaumu polisi nchini Kenya
kwa kutumia vitoa machozi na bunduki kuwalazimisha watu 37 kati ya raia
wake kuingia ndani ya ndege na kusafirishwa hadi China.
Baadhi yao walikuwa wameondolewa mashtaka ya ulaghai. Taiwan inailaumu China kwa kuwateka raia wake na kusema kuwa China iliishinikiza Kenya kuingilia kati mzozo huo wa kidiplomasia.
Kenya haitambui uhuru wa Taiwan na imesema kuwa inafuata sheria ya kuwasafirisha watu kwenda nchini mwao.
China inaitaja Taiwan ambayo imejitawala tangu mwaka 1950 kuwa mkoa wake uliojitenga ambao ni lazima uunganishwe naye.


Post a Comment